Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kutoka 33:18-23

Kutoka 33:18-23 BHN

Mose akasema, “Nakusihi unioneshe utukufu wako.” Mwenyezi-Mungu akamjibu, “Nitapita mbele yako na kukuonesha wema wangu wote nikilitangaza jina langu, ‘Mwenyezi-Mungu’. Mimi nitamrehemu yule ninayependa kumrehemu, na kumhurumia yule ninayependa kumhurumia. Lakini hutaweza kuniona uso maana hakuna mwanadamu yeyote atakayeniona na kuishi.” Kisha Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Kuna mahali karibu nami ambapo utasimama juu ya mwamba; na utukufu wangu utakapokuwa unapita, nitakutia katika pango mwambani na kukufunika kwa mkono wangu, mpaka nitakapokuwa nimepita. Halafu nitauondoa mkono wangu nawe utaniona nyuma, lakini uso wangu hutauona.”

Soma Kutoka 33

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Kutoka 33:18-23