Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kut 33:18-23

Kut 33:18-23 SUV

Akasema, Nakusihi unionyeshe utukufu wako. Akasema, Nitapitisha wema wangu wote mbele yako, nami nitalitangaza jina la BWANA mbele yako; nami nitamfadhili yeye nitakayemfadhili; nitamrehemu yeye nitakayemrehemu. Kisha akasema, Huwezi kuniona uso wangu, maana mwanadamu hataniona akaishi. BWANA akasema, Tazama, hapa pana mahali karibu nami, nawe utasimama juu ya mwamba; kisha itakuwa wakati unapopita utukufu wangu, nitakutia katika ufa wa ule mwamba, na kukufunika kwa mkono wangu hata nitakapokuwa nimekwisha kupita; nami nitaondoa mkono wangu, nawe utaniona nyuma yangu, bali uso wangu hautaonekana.

Soma Kut 33

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Kut 33:18-23