Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mhubiri 11

11
Afanyavyo mwenye busara
1Jishughulishe na biashara
hata kama kwa kubahatisha;
yawezekana baadaye
ukapata chochote kile.
2Wagawie watu saba hata wanane sehemu yako,
maana, hujui balaa litakalofika duniani.
3Mawingu yakijaa maji, mvua hunyesha;
mti ukiangukia kusini au kaskazini,
hapo uangukiapo ndipo ulalapo.
4Anayengoja upepo hatapanda mbegu,
anayesubiri mawingu yatoweke, hatavuna kitu.
5Usivyojua jinsi uhai unavyoingia katika mifupa ya mtoto tumboni mwa mamake,#11:5 au roho iingiavyo katika mimba tumboni mwa mja mzito. kadhalika huwezi kuelewa matendo ya Mungu, ambayo hufanya kila kitu. 6Panda mbegu asubuhi na jioni usiache kupanda, maana, hujui zipi zitaota; za asubuhi, za jioni, au zote zitakuwa nzuri. 7Mwanga wafaa, na kuliona jua kwapendeza macho. 8Mtu akiishi miaka mingi, na aifurahie miaka hiyo yote; lakini akumbuke kuwa siku za giza zitakuwa nyingi, na kwamba yote yatakayofuata ni bure.
Mawaidha kwa vijana
9Ewe kijana, furahia ujana wako, moyo wako, uchangamke wakati ungali kijana. Fuata mapenzi ya moyo wako na upeo wa macho yako. Lakini kumbuka kwamba Mungu atakuhukumu kadiri ya hayo yote. 10Ondoa mahangaiko moyoni mwako, jikinge, usipate maumivu mwilini kwa sababu ujana na mwisho wa maisha ni bure kabisa.

Iliyochaguliwa sasa

Mhubiri 11: BHN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia