Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kumbukumbu la Sheria 32:1-6

Kumbukumbu la Sheria 32:1-6 BHN

“Tegeni masikio enyi mbingu: Sikiliza, ee dunia, maneno ninayosema. Mafundisho yangu na yatone kama mvua, maneno yangu yadondoke kama umande, kama manyunyu kwenye mimea michanga, kama mvua nyepesi katika majani mabichi. Maana nitalitangaza jina la Mwenyezi-Mungu, nanyi mseme, ‘Mungu wetu ni Mkuu’. “Mwenyezi-Mungu ni Mwamba wa usalama; kazi zake ni kamilifu, njia zake zote ni za haki. Yeye ni Mungu mwaminifu asiye na kosa, yeye hufanya mambo ya uadilifu na ya haki. Lakini nyinyi mmekosa uaminifu kwake, nyinyi sio watoto wake tena kwa sababu ya uovu, nyinyi ni kizazi kiovu na kipotovu. Mnawezaje kumlipa hivyo Mwenyezi-Mungu, enyi watu wapumbavu na msio na akili? Je, yeye siye Baba yenu aliyewaumba, aliyewafanya na kuwaimarisha?