Kumbukumbu la Sheria 32:1-6
Kumbukumbu la Sheria 32:1-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Sikilizeni, enyi mbingu, nami nitanena; Na nchi isikie maneno ya kinywa changu. Mafundisho yangu yatadondoka kama mvua, Maneno yangu yatatona-tona kama umande; Kama manyunyu juu ya majani mabichi; Kama matone ya mvua juu ya mimea. Maana nitalitangaza Jina la BWANA; Mpeni ukuu Mungu wetu. Yeye Mwamba, kazi yake ni kamilifu; Maana, njia zake zote ni haki. Mungu wa uaminifu, asiye na uovu, Yeye ndiye mwenye haki na adili. Wametenda mambo ya uharibifu, Hawawi watoto wake, hii ndiyo ila yao; Wao ni kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka. Je! Mnamlipa BWANA hivi, Enyi watu wapumbavu na ujinga? Je! Yeye siye baba yako aliyekununua? Amekufanya, na kukuweka imara.
Kumbukumbu la Sheria 32:1-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Kumbukumbu la Sheria 32:1-6 Biblia Habari Njema (BHN)
“Tegeni masikio enyi mbingu: Sikiliza, ee dunia, maneno ninayosema. Mafundisho yangu na yatone kama mvua, maneno yangu yadondoke kama umande, kama manyunyu kwenye mimea michanga, kama mvua nyepesi katika majani mabichi. Maana nitalitangaza jina la Mwenyezi-Mungu, nanyi mseme, ‘Mungu wetu ni Mkuu’. “Mwenyezi-Mungu ni Mwamba wa usalama; kazi zake ni kamilifu, njia zake zote ni za haki. Yeye ni Mungu mwaminifu asiye na kosa, yeye hufanya mambo ya uadilifu na ya haki. Lakini nyinyi mmekosa uaminifu kwake, nyinyi sio watoto wake tena kwa sababu ya uovu, nyinyi ni kizazi kiovu na kipotovu. Mnawezaje kumlipa hivyo Mwenyezi-Mungu, enyi watu wapumbavu na msio na akili? Je, yeye siye Baba yenu aliyewaumba, aliyewafanya na kuwaimarisha?
Kumbukumbu la Sheria 32:1-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Sikilizeni, enyi mbingu, nami nitanena; Na nchi isikie maneno ya kinywa changu. Mafundisho yangu yatadondoka kama mvua, Maneno yangu yatatona-tona kama umande; Kama manyunyu juu ya majani mabichi; Kama matone ya mvua juu ya mimea. Maana nitalitangaza Jina la BWANA; Mpeni ukuu Mungu wetu. Yeye Mwamba, kazi yake ni kamilifu; Maana, njia zake zote ni haki. Mungu wa uaminifu, asiye na uovu, Yeye ndiye mwenye haki na adili. Wametenda mambo ya uharibifu, Hawawi watoto wake, hii ndiyo ila yao; Wao ni kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka. Je! Mnamlipa BWANA hivi, Enyi watu wapumbavu na ujinga? Je! Yeye siye baba yako aliyekununua? Amekufanya, na kukuweka imara.
Kumbukumbu la Sheria 32:1-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Sikilizeni, enyi mbingu, nami nitanena; Na nchi isikie maneno ya kinywa changu. Mafundisho yangu yatadondoka kama mvua, Maneno yangu yatatona-tona kama umande; Kama manyunyu juu ya majani mabichi; Kama matone ya mvua juu ya mimea. Maana nitalitangaza Jina la BWANA; Mpeni ukuu Mungu wetu. Yeye Mwamba, kazi yake ni kamilifu; Maana, njia zake zote ni haki. Mungu wa uaminifu, asiye na uovu, Yeye ndiye mwenye haki na adili. Wametenda mambo ya uharibifu, Hawawi watoto wake, hii ndiyo ila yao; Wao ni kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka. Je! Mnamlipa BWANA hivi, Enyi watu wapumbavu na ujinga? Je! Yeye siye baba yako aliyekununua? Amekufanya, na kukuweka imara.
Kumbukumbu la Sheria 32:1-6 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Sikilizeni, enyi mbingu, nami nitasema; sikia, ee nchi, maneno ya kinywa changu. Mafundisho yangu na yanyeshe kama mvua, na maneno yangu na yashuke kama umande, kama manyunyu juu ya majani mabichi, kama mvua tele juu ya mimea myororo. Nitalitangaza jina la Mwenyezi Mungu. Naam, sifuni ukuu wa Mungu wetu! Yeye ni Mwamba, kazi zake ni kamilifu, njia zake zote ni haki. Mungu mwaminifu ambaye hakosei, yeye ni mnyofu na mwenye haki. Wamefanya mambo ya upotovu mbele zake; kwa aibu yao, wao si watoto wake tena, lakini ni kizazi kilicho kiovu na kilichopotoka. Je, hii ndiyo njia ya kumlipa Mwenyezi Mungu, enyi watu wajinga na wasio na busara? Je, yeye siye Baba yenu, Muumba wenu, aliyewafanya ninyi na kuwaumba?