1 Mambo ya Nyakati 6:1-30
1 Mambo ya Nyakati 6:1-30 BHN
Lawi alikuwa na wana watatu: Gershomu, Kohathi na Merari. Kohathi alikuwa na wana wanne: Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli. Amramu alikuwa na wana wawili: Aroni na Mose, na binti mmoja jina lake Miriamu. Aroni alikuwa na wana wanne: Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari. Eleazari alimzaa Finehasi, Finehasi akamzaa Abishua, Abishua akamzaa Buki, Buki akamzaa Uzi, Uzi akamzaa Zerahia, Zerahia akamzaa Merayothi, Merayothi akamzaa Amaria, Amaria akamzaa Ahitubu, Ahitubu akamzaa Sadoki, Sadoki akamzaa Ahimaasi, Ahimaasi akamzaa Azaria, Azaria akamzaa Yohanani, na Yohanani akamzaa Azaria. (Azaria ndiye aliyefanya kazi ya ukuhani katika hekalu alilojenga mfalme Solomoni huko Yerusalemu). Azaria alimzaa Amaria, Amaria alimzaa Ahitubu, Ahitubu alimzaa Sadoki, Sadoki alimzaa Meshulamu, Meshulamu alimzaa Hilkia, Hilkia alimzaa Azaria, Azaria alimzaa Seraya, Seraya alimzaa Yehosadaki; Yehosadaki alikwenda uhamishoni wakati Mwenyezi-Mungu alipowapeleka uhamishoni watu wa Yuda na Yerusalemu kwa kuutumia mkono wa mfalme Nebukadneza. Lawi alikuwa na wana watatu: Gershomu, Kohathi na Merari. Kila mmoja wao pia alikuwa na wana. Gershomu aliwazaa Libni na Shimei; Kohathi aliwazaa Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli; naye Merari aliwazaa Mahli na Mushi. Hizi ndizo jamaa za Walawi kulingana na koo zao. Wafuatao ndio wazawa wa Gershomu kutoka kizazi hadi kizazi: Gershomu alimzaa Libni, Libni akamzaa Yahathi, Yahathi akamzaa Zima, Zima akamzaa Yoa, Yoa akamzaa Ido, Ido akamzaa Zera, Zera akamzaa Yeatherai. Hawa ndio wazawa wa Kohathi kutoka kizazi hadi kizazi: Kohathi alimzaa Aminadabu, Aminadabu akamzaa Kora, Kora akamzaa Asiri, Asiri akamzaa Elkana, Elkana akamzaa Ebiasafu, Ebiasafu akamzaa Asiri, Asiri akamzaa Tahathi, Tahathi akamzaa Urieli, Urieli akamzaa Usia, Usia akamzaa Shauli. Wana wa Elkana walikuwa wawili: Amasai na Ahimothi. Na hawa ndio wazawa wa Ahimothi: Ahimothi alimzaa Elkana, Elkana akamzaa Sofai, Sofai akamzaa Nahathi, Nahathi akamzaa Eliabu, Eliabu akamzaa Yerohamu, Yerohamu akamzaa Elkana. Wana wa Samueli walikuwa wawili: Yoeli, mzaliwa wake wa kwanza, na Abiya, mdogo wake. Na hawa ndio wazawa wa Merari kutoka kizazi hadi kizazi: Merari alimzaa Mali, Mali akamzaa Libni, Libni akamzaa Shimei, Shimei akamzaa Uza, Uza akamzaa Shimea, Shimea akamzaa Hagia, Hagia akamzaa Asaya.