Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Nya 6:1-30

1 Nya 6:1-30 SUV

Wana wa Lawi; Gershoni, na Kohathi, na Merari. Na wana wa Kohathi; Amramu, na Ishari, na Hebroni, na Uzieli. Na wana wa Amramu; Haruni, na Musa, na Miriamu. Na wana wa Haruni; Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari. Eleazari akamzaa Finehasi; na Finehasi akamzaa Abishua; na Abishua akamzaa Buki; na Buki akamzaa Uzi; na Uzi akamzaa Zerahia; na Zerahia akamzaa Merayothi, na Merayothi akamzaa Amaria; na Amaria akamzaa Ahitubu; na Ahitubu akamzaa Sadoki; na Sadoki akamzaa Ahimaasi; na Ahimaasi akamzaa Azaria; na Azaria akamzaa Yohana; na Yohana akamzaa Azaria (ndiye huyo aliyefanya kazi ya ukuhani katika nyumba aliyoijenga Sulemani huko Yerusalemu) na Azaria akamzaa Amaria; na Amaria akamzaa Ahitubu; na Ahitubu akamzaa Sadoki; na Sadoki akamzaa Meshulamu; na Meshulamu akamzaa Hilkia; na Hilkia akamzaa Azaria; na Azaria akamzaa Seraya; na Seraya akamzaa Yehosadaki; na Yehosadaki akachukuliwa mateka, hapo BWANA alipowachukua mateka Yuda na Yerusalemu, kwa mkono wa Nebukadreza. Wana wa Lawi; Gershoni, na Kohathi, na Merari. Na haya ndiyo majina ya wana wa Gershoni; Libni, na Shimei. Na wana wa Kohathi walikuwa Amramu, na Ishari, na Hebroni, na Uzieli. Wana wa Merari; Mali, na Mushi. Na hizi ndizo jamaa za Walawi, sawasawa na mbari za baba zao. Wa Gershoni; mwanawe huyo ni Libni, na mwanawe huyo ni Yahathi, na mwanawe huyo ni Zima; na mwanawe huyo ni Yoa, na mwanawe huyo ni Ido, na mwanawe huyo ni Zera, na mwanawe huyo ni Yeatherai. Wana wa Kohathi; mwanawe huyo ni Ishari, na mwanawe huyo ni Kora, na mwanawe huyo ni Asiri; na mwanawe huyo ni Elkana, na mwanawe huyo ni Ebiasafu, na mwanawe huyo ni Asiri; na mwanawe huyo ni Tahathi, na mwanawe huyo ni Urieli, na mwanawe huyo ni Uzia, na mwanawe huyo ni Shauli. Na wana wa Elkana; Amasai, na Ahimothi. Kwa habari za Elkana; wana wa Elkana; mwanawe huyo ni Sufu, na mwanawe huyo ni Tohu; na mwanawe huyo ni Elihu, na mwanawe huyo ni Yerohamu, na mwanawe huyo ni Elkana. Na wana wa Samweli; Yoeli, mzaliwa wa kwanza, na wa pili Abia. Wana wa Merari; Mali, na mwanawe huyo ni Libni, na mwanawe huyo ni Shimei, na mwanawe huyo ni Uza; na mwanawe huyo ni Shimea, na mwanawe huyo ni Hagla, na mwanawe huyo ni Asaya.

Soma 1 Nya 6