Malaki UTANGULIZI
UTANGULIZI
Kitabu cha Malaki huenda kiliandikwa mnamo sehemu ya kwanza ya karne ya 5 K.K., karibu miaka 100 baada ya Waisraeli kurudi nchini mwao kutoka uhamishoni Babuloni.
Miaka thelathini au hamsini kabla ya mahubiri ya Malaki, Waisraeli walikuwa wameitikia mwito wa manabii Hagai na Zekaria kujenga upya hekalu la Yerusalemu (520-515 K.K.). Lakini kidogo kidogo tazamio lao la hali mpya chini ya uongozi wa mtawala Zerubabeli lilianza kufifia. Hali ya kidini na maisha adili ilianza kufifia: Ibada kwa Mungu ikasahauliwa (1:6-14), makuhani wakazembea katika huduma yao, nayo sheria ya Mungu ikawa inapuuzwa (2:1-16). Hali hiyo ilimfanya nabii huyu Malaki kuwahimiza watu wafanye mabadiliko thabiti na ya kimsingi katika maisha yao kwa kuwakumbusha upendo wa Mungu (1:1-5) na pia kwamba adhabu yake iko karibu (2:17–3:5; 3:13–4:6). Aliwatangazia kwamba Mungu atamtuma mtumishi wake (3:10) ambaye atakuwa nabii kama Elia (4:5). Katika Injili – Agano Jipya, ahadi hiyo inaoneshwa kukamilika katika huduma ya Yohane Mbatizaji ambaye alikuwa na jukumu la kutayarisha ujio wa Yesu Kristo (Mat 17:11-13; Luka 1:17).
Iliyochaguliwa sasa
Malaki UTANGULIZI: BHND
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote (Yenye Vitabu vya Deuterokanoni): Tafsiri ya Ushirikiano wa Makanisa (BHN): Hakimiliki -1995, 2001: kwa Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.
Jifunze Mengi Kuhusu Biblia Habari Njema