Yohana 18
18
Kuchongewa na Yuda.
1Yesu alipokwisha kuyasema haya akatoka pamoja na wanafunzi wake kwenda ng'ambo ya kijito cha Kidoroni, kulikokuwa na kiunga. Humo wakaingia yeye na wanafunzi wake.#2 Sam. 15:23; Mat. 26:36; Mar. 14:32; Luk. 22:39.
(2-11: Mat. 26:47-56; Mar. 14:43-52; Luk. 22:47-53.)
2Lakini naye Yuda aliyemchongea alipajua hapo, kwani Yesu na wanafunzi wake walikusanyika mara nyingi hapo.#Luk. 21:37. 3Basi, Yuda alipokwisha kupata kikosi cha askari na watumishi wa watambikaji wakuu na wa Mafariseo, akaenda kulekule, wakishika taa na mienge na selaha. 4Yesu alipoyajua yote yatakayomjia akawatokea, akawauliza: Mwamtafuta nani?#Yoh. 19:28. 5Walipomjibu: Yesu wa Nasareti, akawaambia: Ni mimi. Lakini naye Yuda mwenye kumchongea alikuwa amesimama pamoja nao. 6Alipowaambia: Ni mimi, wakarudi nyuma, wakaanguka chini. 7Alipowauliza tena: Mwamtafuta nani? wakasema: Yesu wa Nasareti. 8Yesu akajibu: Nimekwisha waambia: Ni mimi; mkinitafuta mimi, waacheni hawa, waende zao! 9Imekuwa hivyo, litimie lile neno, alilolisema: Wale, ulionipa, sikuwaangamiza hata mmoja.#Yoh. 17:12. 10Simoni Petero alikuwa na upanga, akauchomoa, akampiga mtumwa wa mtambikaji mkuu, akamkata sikio la kuume; jina lake yule mtumwa ndiye Malko. 11Lakini Yesu akamwambia Petero: Uchomeke upanga alani mwake! Kinyweo, Baba alichonipa, nisikinywe?#Mat. 26:39.
Kukana kwa Petero.
(12-27: Mat. 26:57-75; Mar. 14:53-72; Luk. 22:54-71.)
12Kisha kikosi cha askari na mkubwa wao na watumishi wa Wayuda wakamkamata Yesu, wakamfunga. 13Wakampeleka kwanza kwa Ana; kwani alikuwa mkwewe Kayafa aliyekuwa mtambikaji mkuu wa mwaka ule. 14Kayafa ndiye yule aliyekula njama na Wayuda kwamba: Inafaa, mtu mmoja afe kwa ajili ya watu.#Yoh. 11:49-50. 15Lakini Simoni Petero na mwanafunzi mwingine wakamfuata Yesu; yule mwanafunzi mwingine alikuwa amejuana na mtambikaji mkuu, akaingia pamoja na Yesu uani kwa mtambikaji mkuu, 16Petero akasimama nje mlangoni. Yule mwanafunzi mwingine aliyejuana na mtambikaji mkuu akatoka, akasema na mlinda mlango, akamwingiza Petero. 17Kisha kijakazi aliyekuwa mlinda mlango alipomwambia Petero: Wewe nawe humo miongoni mwao wanafunzi wa mtu huyo? akasema: Simo. 18Lakini watumwa na watumishi walikuwa wamewasha moto wa makaa, kwani palikuwa na baridi, wakasimama, wakaota moto; naye Petero alisimama pamoja nao, akiota moto.
Yesu mbele ya Ana.
19Mtambikaji mkuu alipomwuliza Yesu kwa ajili ya wanafunzi wake na kwa ajili ya mafundisho yake, 20Yesu akamjibu: Mimi nimesema waziwazi ulimwenguni. Mimi siku zote nimefundisha nyumbani mwa kuombea napo Patakatifu, Wayuda wote wanapokusanyika; hakuna, nililolisema na kufichaficha,#Yoh. 7:14,26. 21Unaniulizaje? Uwaulize walionisikia, niliyowaambia! Tazama, hao wanayajua, niliyoyasema mimi. 22Aliposema hivyo, mtumishi mmoja aliyesimama hapo akampiga Yesu kofi akisema: Mtambikaji mkuu unamjibu hivyo? 23Yesu akamjibu: Kama nimesema maovu, ujulishe huo uovu! Lakini kama nimesema vema, unanipigia nini? 24Basi, Ana akampeleka kwa mtambikaji mkuu Kayafa hivyo, alivyokuwa amefungwa.
Jogoo anawika.
25Lakini Simoni Petero alikuwa amesimama akiota moto. Walipomwuliza: Wewe nawe humo miongoni mwao wanafunzi wake? akakana akisema: Simo. 26Miongoni mwao watumwa wa mtambikaji mkuu mlikuwamo mmoja aliyekuwa ndugu yake yule, Petero aliyemkata sikio, akasema: Mimi sikukuona kule kiungani pamoja naye? 27Petero akakana tena; mara hiyo jogoo akawika.
Yesu mbele ya Pilato.
(28—19:15: Mat. 27:2,11-30; Mar. 15:1-19; Luk. 23:1-25.)
28Wakamtoa Yesu kwa Kayafa, wakampeleka bomani kulipokucha. Wao wenyewe hawakuingia bomani kwa mwiko wao, wasijitie uchafu, wapate kula Pasaka. 29Kwa hiyo Pilato akawatokea nje, akauliza: Mwaleta mashtaka gani ya mtu huyu? 30Walipojibu wakimwambia: Huyu kama asingekuwa mwenye kufanya maovu, tusingemleta kwako, 31Pilato akawaambia: Mchukueni ninyi, mmhukumu kwa Maonyo yenu! Wale Wayuda wakamwambia: Sisi hatuna ruhusa ya kuua mtu.#Yoh. 19:6-7. 32Ilikuwa hivyo, litimie lile neno, Yesu alilolisema na kuonyesha kufa kulikomngoja.#Yoh. 12:32-33; Mat. 20:19.
33Pilato akaingia tena bomani, akamwita Yesu, akamwuliza: Wewe ndiwe mfalme wa Wayuda? 34Yesu akajibu: Wasema hivi kwa mawazo yako mwenyewe, au wako wengine waliokusimulia mambo yangu? 35Pilato akajibu: Je? Mimi Myuda? Wao wa taifa lako na watambikaji wakuu wamekuleta kwangu. Umefanya nini? 36Yesu akajibu: Ufalme wangu sio wa ulimwengu huu. Kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu, watumishi wangu wangeupigania, nisitiwe mikononi mwa Wayuda. Lakini sasa ufalme wangu sio wa hapa. 37Pilato akamwuliza: Basi, wewe u mfalme gani? Yesu akajibu: Wewe unavyosema, ndivyo: mimi ni mfalme. Niliyozaliwa, tena niliyojia ulimwenguni, ndiyo hii: niishuhudie iliyo ya kweli! Kila aliye na kweli huisikia sauti yangu.#1 Tim. 6:13. 38Pilato akamwambia: Iliyo ya kweli ndiyo nini? Alipokwisha kuyasema haya akawatokea tena Wayuda, akawaambia: Mimi sioni kwake neno la kumhukumu. 39Lakini iko desturi kwenu, niwafungulie mmoja siku ya Pasaka; basi, mwataka, niwafungulie mfalme wa Wayuda? 40Ndipo, walipopiga makelele tena wakisema: Huyu hatumtaki, twamtaka Baraba; naye Baraba alikuwa mnyang'anyi.
Iliyochaguliwa sasa
Yohana 18: SRB37
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.