Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Matendo ya Mitume 16

16
Timoteo.
1Akafika Derbe na Listira; huko kulikuwa na mwanafunzi, jina lake Timoteo, mwana wa mwanamke wa Kiyuda aliyemtegemea Bwana, lakini baba alikuwa Mgriki.#Tume. 17:14; 19:22; 2 Tim. 1:5. 2Kwa kuwa huyo alishuhudiwa vema na ndugu waliokuwamo mle Listira na Ikonio,#Tume. 6:3. 3Paulo alimtaka, aondoke kwenda naye. Akamchukua, akamtahiri kwa ajili ya Wayuda waliokuwa katika miji ile, kwani wote walimjua, ya kuwa baba yake alikuwa Mgriki. 4Walipozunguka katika miji ile wakawafundisha kuishika ile miiko iliyoagizwa nao mitume na wazee wa Yerusalemu.#Tume. 15:23-29. 5Hivyo wateule wakapata nguvu za kumtegemea Bwana, wakawa wengi zaidi kwa kuongezwa kila siku.
Wito wa kuja Ulaya.
6Wakaikata nchi ya Furigia na ya Galatia wakikatazwa na Roho Mtakatifu, wasiliseme Neno lao katika Asia.#Tume. 18:23. 7Walipofika Misia, wakajaribu kwenda Bitinia, lakini Roho wa Yesu hakuwapa ruhusa. 8Basi wakapita Misia, wakatelemka, wakafika Tiroa.
9*Huko Paulo akatokewa na njozi usiku, akaona mtu wa Makedonia, amesimama na kumbembeleza kwamba: Vuka, uje Makedonia, utusaidie! 10Alipokwisha kuiona njozi hiyo, papo hapo tukatafuta, jinsi tutakavyovuka, tuje Makedonia, maana sote tumejua kweli, ya kuwa ni Mungu aliyetuita, tuje, tuwapigie hiyo mbiu njema.
Lidia.
11Tukaondoka Tiroa, tukaingia chomboni, tukaenda kwa tanga moja Samotirake; kesho yake tukafika Mji Mpya. 12Toka huko tukafika Filipi, ni mji wa mbele wa upande huo wa Makedonia, tena ndimo, Waroma walimotua. Tulipokuwa tumekaa mjini mle siku kidogo 13tukatoka langoni kwenda nje siku ya mapumziko, tukaenda kando ya mto, tulipowazia kuwa pao pa kuombea. Ndipo, tulipokaa, tukisema na wanawake waliokusanyika. 14Palikuwapo mwanamke, jina lake Lidia; alitoka mji wa Tiatira, akawa mchuuzi wa nguo za kifalme. Kwa sababu alimcha Mungu, akasikiliza. Naye Bwana akamfunulia moyo, ayashike yaliyosemwa na Paulo.#Yoh. 6:44. 15Alipokwisha kubatizwa pamoja nao waliokuwamo mwake akatubembeleza na kusema: Kama mmeniona mimi kwamba: Ni mwenye kumtegemea Bwana, mwingie mwangu, mkae! Ndivyo, alivyotushurutisha.*
Kijakazi mwenye pepo.
16*Ikawa, sisi tulipokwenda kuomba, tukakutana na kijakazi mwenye pepo ya kuagua. Naye aliwachumia mabwana zake mali nyingi na uaguzi wake.#Tume. 19:24. 17Pote, tulipokwenda, akatufuata, Paulo na sisi, akapaza sauti akisema: Watu hawa ndio watumwa wake Mungu alioko huko juu, nao huwatangazia njia ya wokovu.#Mar. 1:24,34. 18Alipovifanya siku nyingi, vikamwumiza Paulo, akageuka, akamwambia yule pepo: Nakuagiza wewe kwa Jina la Yesu Kristo, umtoke! Naye akamtoka saa ileile.#Mar. 16:17. 19Lakini mabwana zake walipoona, ya kuwa chumo lao la mali limewapotea, wakamshika Paulo na Sila, wakawaburura, wakaenda nao sokoni kwa wakubwa wa mji. 20Wakawapeleka kwa mabwana wakubwa, wakasema: Watu hawa wanauchafua mji wetu; ni Wayuda,#Tume. 17:6; 1 Fal. 18:17. 21hufundisha desturi zilizo mwiko kwetu kuzipokea au kuzifanya sisi tulio Waroma. 22Watu wengi walipoinuka kuwaendea kwa nguvu, mabwana wakubwa wakawapokonya mavazi yao, wakaagiza, wapigwe.#2 Kor. 11:25; Fil. 1:30; 1 Tes. 2:2. 23Walipokwisha kuwapiga viboko vingi wakawatia kifungoni, wakamwagiza mlinda kifungo, awatie mahali pasipoingilikana. 24Naye alipolipata agizo hili akawatia katika chumba cha ndani kabisa, tena miguu yao akaitia mikatale.
Mlinda kifungo wa Filipi.
25Lakini usiku wa manane Paulo na Sila wakamwomba Mungu na kumwimbia, wafungwa wenzao wakiwasikiliza. 26Papo hapo nchi ikatetemeka sana, hata misingi ya kifungo ikatikisika; mara milango yote ikafunguka, hata minyororo yao wote ikakatika. 27Mlinda kifungo akazinduka, akaona, milango ya kifungo iko wazi, akachomoa upanga, akataka kujiua, kwani alidhani, wafungwa wametoroka. 28Lakini Paulo akamkemea na kupaza sauti akisema: Usijifanyie kiovu! Kwani sisi sote tupo hapa. 29Akaagiza, taa ije, akarukia ndani na kutetemeka, akamwangukia Paulo na Sila. 30Alipowapeleka nje na kuwauliza: Bwana zangu, inayonipasa kuyafanya, nipate kuokoka ndiyo nini?#Tume. 2:37. 31wakasema: Mtegemee Bwana Yesu! Ndivyo, utakavyookoka wewe nao waliomo nyumbani mwako. 32Wakamwambia Neno lake Mungu yeye nao wote waliokuwamo mwake.* 33Akawakaribisha saa ileile ya usiku, akawaosha madonda ya mapigo yao, akabatizwa papo hapo yeye nao wote waliokuwa wake. 34Kisha akawaingiza mwake, akawaandalia meza, akashangilia yeye nao wa nyumbani mwake wote, ya kuwa wamepata kumtegemea Mungu.
35Kulipokucha, mabwana wakubwa wakawatuma wale askari waliowapiga, wamwambie: Wafungue watu wale! 36Mlinda kifungo alipomwambia Paulo maneno haya kwamba: Mabwana wakubwa wametuma watu, mfunguliwe; sasa tokeni mwende na kutengemana! 37Paulo akawaambia: Wametupiga mbele ya watu pasipo kutuhukumu sisi tulio Waroma na kututia kifungoni. Sasa je? Wanataka kutukimbiza na kufichaficha? Sivyo, sharti waje wenyewe, watutoe!#Tume. 22:25. 38Askari waliowapiga walipowaambia mabwana wakubwa maneno haya, wakashikwa na woga kwa kusikia, ya kuwa ndio Waroma. 39Wakaja, wakawabembeleza, wakawatoa, wakawaomba sana, watoke mjini mle. 40Ndipo, walipotoka kifungoni, wakaingia nyumbani mwa Lidia; walipokwisha kuonana na ndugu na kuwatuliza mioyo wakaondoka.

Iliyochaguliwa sasa

Matendo ya Mitume 16: SRB37

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

Video ya Matendo ya Mitume 16