Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Matendo ya Mitume 12

12
Kufunguliwa kwake Petero.
1Siku zile mfalme Herode alikuwa amekamata wengine miongoni mwao wateule, awafanyizie maovu.#Tume. 4:3. 2Akamwua Yakobo, ndugu yake Yohana, kwa upanga. 3Alipoona, ya kuwa Wayuda wamependezwa, akaendelea, akamkamata naye Petero, siku za mikate isiyochachwa zilipotimia. 4Alipokwisha kumkamata akamtia kifungoni, akaagiza vikosi vinne, kila kikosi cha askari wanne, wamlinde kwa zamu, akataka kumtia mikononi mwa watu, siku za Pasaka zitakapokuwa zimepita. 5Petero alipolindwa hivyo kifungoni, wateule wakamwombea kwa Mungu pasipo kuchoka. 6Lakini hapo, Herode alipotaka kumtoa, usiku uleule Petero alikuwa amelala katikati ya askari wawili akiwa amefungwa na mapingu mawili; nao walinzi walikilinda kifungo mlangoni. 7Mara malaika wa Bwana akasimama hapo karibu, nao mwanga ukamulika chumbani. Akamwamsha Petero kwa kumpiga ubavu akisema: Inuka upesi! Ndipo, mapingu yalipomwanguka mikononi.#Tume. 5:19. 8Kisha malaika akamwambia: Jifunge nguo zako, uvae navyo viatu vyako! Alipokwisha kufanya hivyo, akamwambia tena: Jivike kanzu yako, unifuate! 9Kisha akatoka akimfuata, asijue, kama ni kweli yaliyofanyika na malaika; maana aliwaza, ameona njozi. 10Wakapita zamu ya kwanza ya walinzi na ya pili, wakalifikia lango la chuma linaloelekea mjini, nalo likawafungukia lenyewe, wakatoka; walipoendelea njia tu, papo hapo ndipo, malaika alipoondoka na kumwacha.
11Naye Petero, moyo wake ulipomrudia, akasema: Sasa nimejua kweli ya kuwa Bwana amemtuma malaika wake, akaniokoa katika mkono wa Herode na katika mangojeo yote ya watu wa kwao Wayuda. 12Alipokuwa akiyawaza hayo akaifikia nyumba ya Maria, mama yake Yohana anayitwa Marko; ndimo, wengi walimokuwa wamekusanyikia kuomba.#Tume. 15:37. 13Alipogonga kilango kilichomo langoni, akaja kijakazi kusikiliza, jina lake Rode. 14Naye alipoutambua mtamko wa Petero hakulingua lango kwa furaha, ila akaingia mbio, akawaambia, ya kuwa Petero amesimama langoni. 15Nao wakamwambia: Una wazimu. Lakini alipokaza kusema, ya kuwa ndivyo, wakasema: Ni malaika wake.#Luk. 24:37. 16Petero alipofuliza kugonga, wakamfungulia, wakamwona, wakashangaa sana. 17Akawapungia mkono, wanyamaze; kisha akawasimulia, jinsi Bwana alivyomtoa kifungoni, akasema: Habari wapasheni nao akina Yakobo nao walio ndugu! Kisha akatoka, akaenda mahali pengine.
Kufa kwake Herode.
18Palipokucha, pakapatikana mahangaiko mengi kwa askari, wasijue, jinsi ya Petero yalivyowezekana.#Tume. 5:21-22. 19Naye Herode asipompata hapo, alipomtaka, akawaulizauliza walinzi, akaagiza, wafungwe. Kisha akaondoka Yudea, akatelemka kwenda Kesaria, akatua huko. 20Lakini moyoni alifikiri kuwashambulia watu wa Tiro na Sidoni; ndipo, walipomwendea wote pamoja, wakamhonga Bulasto aliyekuwa mshika funguo wa mfalme, wakamwomba, awaamue, kwa sababu walichuma vyakula vyao katika nchi ya mfalme.#1 Fal. 5:11; Ez. 27:17. 21Siku, waliyopatania, Herode akavaa nguo ya kifalme, akakaa katika kiti cha uamuzi, akatoa maneno. 22Watu walipoitikia kwamba: Ni Mungu, tunayemsikia, si mtumtu tu,#Ez. 28:2. 23papo hapo malaika wa Bwana akampiga, kwa sababu hakumpa Mungu utukufu. Akawa akiliwa na vidudu, akakata roho.#Dan. 5:20.
24Lakini Neno la Bwana likakua na kuenea pengi.#Tume. 6:7; Yes. 55:11. 25Barnaba na Sauli walipoimaliza kazi yao wakarudi toka Yerusalemu wakimchukua naye Yohana aliyeitwa Marko#Tume. 11:29-30; 12:12; 15:37.

Iliyochaguliwa sasa

Matendo ya Mitume 12: SRB37

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia