Matendo ya Mitume 13
13
Safari ya kwanza ya Paulo.
1Katika wateule waliokuwamo Antiokia walikuwa wafumbuaji na wafunzi, akina Barnaba na Simeoni aliyeitwa Nigeri na Lukio wa Kirene na Manaeni aliyelelewa pamoja na mfalme Herode, tena Sauli.#Tume. 11:27. 2Hao walipokuwa wakimtumikia Bwana na kufunga, Roho Mtakatifu akasema: Nitengeeni Barnaba na Sauli, waifanye kazi, niliyowaitia!#Tume. 9:15. 3Ndipo, walipofunga na kuomba, wakawabandikia mikono, kisha wakawasindikiza.#Tume. 14:23; 6:6.
Elima.
4Kwa hivyo, walivyotumwa na Roho Mtakatifu, wakatelemka kwenda Seleukia; huko wakaingia chomboni kwenda Kipuro. 5Walipofika Salami wakalitangaza Neno la Mungu katika nyumba za kuombea za Wayuda. Naye Yohana alikuwa pamoja nao akiwatumikia.#Tume. 12:12,25. 6Wakakikata kisiwa chote wakienda kwa miguu mpaka Pafo, hapo wakaona mtu wa Kiyuda aliyekuwa mganga na mwaguaji wa uwongo, jina lake Baryesu. 7Huyo alikaa kwa mtawala nchi Sergio Paulo aliyekuwa mtu mwelekevu. Alipomwita Barnaba na Sauli kwa kutaka kulisikia Neno la Mungu, 8yule mganga Elima (kwani hii ndiyo maana ya jina lake) akawabishia mno akitaka kumpinga mtawala nchi, asije kumtegemea Mungu.#2 Tim. 3:8. 9Lakini Sauli anayeitwa Paulo akajaa Roho takatifu, akamkazia macho, 10akasema: Wewe mwana wa Msengenyaji, uliyejaa udanganyi na uovu wote, unachukizwa na wongofu wote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyoka? 11Sasa utaona, mkono wa Bwana ukikukamata! Utakuwa kipofu, usilione jua siku hizi! Papo hapo akaguiwa na kiwi cha macho na giza, akapapasapapasa akitafuta watu wa kumshika mkono. 12Mtawala nchi alipoyaona yaliyofanyika, akaustaajabu huo ufundisho wa Bwana, akamtegemea.
Antiokia katika Pisidia.
13Kisha Paulo na wenziwe wakajipakia chomboni, wakaondoka Pafo kwenda Perge katika Pamfilia; lakini Yohana akawaacha, akarudi Yerusalemu.#Tume. 15:38. 14Walipoondoka Perge, wakakata nchi, wakafika Antiokia wa Pisidia; siku ya mapumziko wakaingia nyumbani mwa kuombea, wakakaa. 15Mafungu ya Maonyo na ya Wafumbuaji yalipokwisha kusomwa, wakubwa wa nyumba ya kuombea wakatuma kwao kwamba: Ndugu zetu, mkiwa na neno la kuituliza mioyo ya watu lisemeni!#Tume. 15:21. 16Ndipo, Paulo alipoinuka, akawapungia mkono, akasema: Waume wa Isiraeli, nanyi mnaomcha Mungu, sikilizeni! 17Mungu wa watu hawa wa kwetu Waisiraeli aliwachagua baba zetu, akawakuza kuwa makundi makubwa, walipokaa ugenini katika nchi ya Misri. Kisha akaunyosha mkono wake, akawaongoza na kuwatoa kule,#2 Mose 6:6; 12:37,41; 14:8; Yes. 1:2. 18akawavumilia jangwani miaka kama 40.#2 Mose 16:35; 4 Mose 14:34; 5 Mose 1:31. 19Alipokwisha poteza mataifa saba katika nchi ya Kanaani, akawapa nchi yao, waitwae.#5 Mose 7:1; Yos. 14:2. 20Kisha akawapa waamuzi miaka kama 450, mpaka siku za mfumbuaji Samueli.#Amu. 2:16; 1 Sam. 3:20. 21Walipotaka mfalme, Mungu akawapa Sauli, mwana wa Kisi, mtu wa shina la Benyamini, miaka 40.#1 Sam. 8:5; 10:21,24. 22Tena alipokwisha kumwondoa huyo akamwinua Dawidi, awe mfalme wao; mwenyewe akamshuhudia kwamba: Nimemwona Dawidi, mwana wa Isai, kuwa mtu anayeupendeza moyo wangu; ndiye atakayeyafanyiza yote, niyatakayo.#1 Sam. 13:14; 16:12-13; Sh. 89:21. 23Katika uzao wake huyo Mungu akawaletea Waisiraeli mwokozi Yesu, kama alivyoagana nao.#2 Sam. 7:12; Yes. 11:1. 24Alipokuwa hajawatokea bado, Yohana alikwisha kuwatangazia watu wote wa Isiraeli ubatizo wa kujutisha.#Luk. 3:3. 25Lakini Yohana alipoumaliza mwenendo wake akasema: Yeye, mnayeniwazia kuwa, mimi siye; lakini tazameni, anakuja nyuma yangu, ambaye hainipasi kumfungulia viatu vya miguu yake.#Mar. 1:7; Luk. 3:16; Yoh. 1:20,27. 26Waume ndugu zangu, wana wa uzao wa Aburahamu, nanyi mnaomcha Mungu, Neno la wokovu huu lilitumwa kufika kwetu sisi;#Tume. 13:46. 27lakini wale wanaokaa Yerusalemu na wakubwa wao hawakumtambua huyo, wakamhukumu; ndivyo, walivyoyatimiza maneno ya Wafumbuaji yanayosomwa kila siku ya mapumziko.#Yoh. 16:3. 28Ijapokuwa hawakuona neno lolote la kumwua, wakamhimiza Pilato, aangamizwe.#Mat. 27:22-23. 29Nao walipokwisha kuyatimiza yote, aliyoandikiwa, wakamwambua mtini, wakamzika kaburini;#Mat. 27:59-60. 30lakini Mungu akamfufua katika wafu.#Tume. 3:15. 31Kisha siku nyingi akaonekana kwao waliotoka pamoja naye Galilea kwenda kupanda Yerusalemu. Hao sasa ndio mashahidi wake kwenye watu wa kwetu.#Tume. 1:3. 32Nasi tunawapigia mbiu njema ya kile kiagio, baba zetu walichokipata kwamba:#Tume. 13:23. 33Mungu amekitimizia wana wetu alipomfufua Yesu. ndivyo, alivyoandikwa hata katika shangilio la pili:
Wewe ndiwe Mwanangu, siku hii ya leo mimi nimekuzaa.#Sh. 2:7.
34Lakini ya kuwa amemfufua katika wafu, asirudie tena kuoza, ndivyo, alivyosema kwamba:
Nitawapa ninyi magawio matakatifu ya Dawidi
yanayotegemeka.#Yes. 55:3. 35Kwa hiyo anasema hata pengine:
Hutamtoa akuchaye, apate kuoza.#Sh. 16:10. 36Lakini Dawidi alipokwisha kuwatumikia waliokuwako siku zile kwa mapenzi yake Mungu, alipata kulala, akawekwa mahali pa baba zake, akapata kuoza.#Tume. 2:29. 37Lakini yule Mungu aliyemfufua, hakupa kuoza. 38Kwa hiyo waume ndugu, litambulkane kwenu, ya kuwa ni kwa ajili yake yeye, mkipigiwa mbiu ya kwamba: Makosa yameondolea!#Tume. 10:43; 4 Mose 15:30; Rom. 8:3-4. 39Na tena: Yote yasiyowezekana kuondolewa kwa nguvu ya Maonyo ya Mose, kila mwenye kumtegemea Bwana anaondolewa nayo kwa nguvu yake yeye, awe mwongofu.#Rom. 10:4. 40Kwa hiyo angalieni, ninyi yasiwajie yaliyosemwa na Wafumbuaji ya kuwa:#Hab. 1:5.
41Ninyi wenye kubeza, angalieni na kustaajabu, mzizimke!
Kwani mimi siku hizi nitatenda tendo,
kama mtu angewasimulia tendo hilo, msingeliitikia.
42Walipotoka hapo, wamizimu wakawaomba, nao waambiwe maneno hayo siku ya pili ya mapumziko. 43Waliokuwamo nyumbani mwa kuombea walipotawanyika, Wayuda na wafuasi wengi waliomcha Mungu wakamfuata Paulo na Barnaba. Waliposema nao wakawahimiza, washikamane na magawio yake Mungu.#Tume. 11:23. 44Siku ya mapumziko iliyofuata walikusanyika wao wa mji wote, walisikie Neno la Mungu. 45Lakini Wayuda walipoyaona hayo makundi ya watu wakajazwa wivu, wakayabisha yaliyosemwa na Paulo na kumtukana.#Tume. 14:2; 13:50. 46Ndipo, Paulo na Barnaba waliposema waziwazi pasipo woga: Ilikuwa imepasa, ninyi mwambiwe wa kwanza Neno la Mungu. Lakini mnapolitupa na kujiwazia kwamba: Uzima wa kale na kale hauwafalii, basi, twawageukia wamizimu.#Tume. 3:26; 28:25-28; Mat. 10:5-6; Luk. 7:30. 47Kwani tumeagizwa hivyo na Bwana:
Nimekuweka kuwa mwanga wa wamizimu,
uwe wokovu wao hata mapeoni kwa nchi.#Yes. 49:6. 48Wamizimu walipoyasikia haya wakafurahi, wakalitukuza Neno la Bwana, wakalitegemea wote waliokuwa wamewekewa kupata uzima wa kale na kale.#Rom. 8:29-30. 49Ndivyo, Neno la Bwana lilivyoenea katika nchi ile yote. 50Lakini Wayuda waliwachokoza wanawake wakuu walioyashika matambiko yao, hata wakubwa wa mji, wakawachukua, wawashambulie akina Paulo na Barnaba, wakawafukuza, watoke mipakani kwao. 51Ndipo, walipowakung'utia mavumbi ya miguuni, wakaenda, wakaja Ikonio.#Tume. 18:6; Mat. 10:14; Luk. 9:5. 52Lakini wanafunzi wakajazwa furaha na Roho takatifu.
Iliyochaguliwa sasa
Matendo ya Mitume 13: SRB37
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.