Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Luka MT. 14

14
1IKAWA, Yesu alipoingia katika nyumba ya mtu mmoja, mtu mkuu katika Mafarisayo, siku ya sabato, ale chakula, walikuwa wakimvizia. 2Bassi mbele yake palikuwa mtu hawezi safura. 3Yesu akajibu akawaambia wana sharia na Mafarisayo, akisema, Je? ni halali kuponya siku ya sabato, ama sivyo? Wakanyamaza. 4Akamtwaa, akamponya, akamrukhusu. 5Akajibu akawaambia, Nani wenu mwenye punda au ngʼombe ametumbukia kisimani, asiyemwondoa marra moja siku ya sabato? 6Nao hawakuweza kumjibu kwa haya. 7Akawaambia mfano wale waliokwitwa, alipoona jinsi walivyochagua viti vya kwanza; akiwaambia, 8Ukiitwa na mtu arusini, usiketi katika kiti cha kwanza, isiwe labda mwenye sifa kupita zako amekwitwa nae, 9akaja mwenye kuwaiteni wewe nae, akakuambia, Mpishe huyu; ndipo utaanza kwa aibu kutwaa pahali pa chini. 10Walakini ukiitwa, enenda ukaketi pahali pa chini: illi akija yeye aliyekuita akuamhie, Rafiki yangu, jongea huku mbele; ndipo utakapokuwa na heshima machoni pao wote waketio pamoja nawe. 11Kwa maana killa ajikwezae atadhilika; nae ajidhiliye atakwezwa.
12Akamwambia na yule aliyemwalika, Ufanyapo chakula cha assubuhi au cha jioni, usiwaite rafiki zako, wala ndugu zako, wala jamaa zako, wala jirani zako walio na mali, wasije na wao wakakualika wewe, ukapata malipo. 13Bali ufanyapo karamu, wakaribishe maskini, vilema, viwete, vipofu: nawe utakuwa kheri: 14kwa sababu hawana kitu cha kukulipa; maana utalipwa katika ufufuo wa wenye haki.
15Bassi mtu mmoja katika hawo walioketi pamoja nae, alipoyasikia haya, akamwambia, Yu kheri atakaekula mkate katika ufalme wa Mungu. 16Akamwambia, Mtu mmoja alifanya karamu kubwa, akaalika watu wengi, 17akamtuma mtumishi wake saa ya karamu kwenda kuwaambia walioalikwa, Njoni, maana vitu vyote vimekwisha kuwa tayari. 18Wakaanza kutoa udhuru, wote pia kwa nia moja. Wa kwanza akamwambia, Nimenunua shamba, sina buddi kwenda na kulitazama; nakuomba, unisamehe. 19Mwingine akasema, Nimenunua ngʼombe, jozi tano: naenda niwajaribu; nakuomba unisamehe. 20Mwingine akasema, Nimeoa mke, na kwa sababu hii siwezi kuja. 21Yule mtumishi akaenda, akamwarifu Bwana wake mambo haya. Ndipo yule mwenye nyumba akaghadhabika, akamwambia mtumishi wake, Toka upesi ukaende njia kuu na vichochoro vya mji, ukalete hapa maskini, na vilema, na viwete, na vipofu. 22Yule mtumishi akasema, Yamekwisha kutendeka hayo uliyoniagiza na ingaliko nafasi. 23Yule Bwana akamwambia mtumishi wake, Kaenda barabarani na mipakani, ukawashurutishe waingie illi nyumba yangu ipate kujaa. 24Maana nawaambieni ya kwamba katika watu wale walioalikwa hapana hatta mmoja atakaeionja karamu yangu. 25Bassi makutano mengi wakafuatana nae; akageuka akawaambia, 26Mtu akija kwangu, nae hamehukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake wanaume na wanawake, na uzima wake pia, hawezi kuwa mwanafunzi wangu. 27Na mfu ye yote asiyechukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu. 28Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza na kuihesabu gharama kama ana vitu vya kuumaliza? 29Asije akawa hawezi kuumaliza baada ya kuweka msingi, watu wote wakaanza kumdhihaki, wakisema, 30Mtu huyu alianza kujenga, akawa hana nguvu za kumaliza. 31Au mfalme gani, kama anakwenda kupigana na mfalme mwingine, asiyeketi kwanza na kufanya shauri kwamba yeye pamoja na watu elfu kumi ataweza kukutana nae anaemjia pamoja na watu elfu ishirini? 32Kama sivyo, hutuma ujumbe kutaka sharti za amani, yule mtu akiwa angali mbali. 33Bassi, kadhalika killa mmoja wenu asiyeviacha vitu vyote alivyo navyo hawezi kuwa mwanafunzi wangu. 34Chumvi ni njema, illakini ile chumvi ikiwa imeharibika, itatiwa nini ikolee? 35Haiifai inchi wala jaa; watu huitupa nje. Mwenye masikio ya kusikilia, na asikie.

Iliyochaguliwa sasa

Luka MT. 14: SWZZB1921

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia