Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Luka MT. 13

13
1WAKATI huohuo walikuwapo watu wakimwarifu khabari za Wagalilaya wale ambao Pilato alichanganya damu yao na dhabihu zao. 2Akajibu, akawaambia, Je! Mwadhani ya kuwa Wagalilaya hawo walikuwa wenye dhambi kuliko Wagalilaya wote hatta wakapata mateso kama hayo? 3Nawaambieni sivyo: lakini msipotuhu nyote mtaangamia vivyo hivyo. 4Au wale kumi na wanane walioangukiwa na mnara katika Siloam, ukawaangamiza, mwadhani ya kuwa walikuwa wakosaji kuliko watu wote wakaao Yerusalemi? 5Nawaanibieni, Sivyo: lakini msipotubu, nyote mtaangamia vivyo hivyo. 6Akanena mfano huu: Mtu mmoja alikuwa na mtini, umepandwa katika shamba lake la mizabibu; akaenda akitafuta matunda juu yake wala hakupata. 7Akamwambia mtunzaji wa shamba la mizabibu, Tazama, miaka mitatu hii naja nikitafuta matunda katika mtini huu, nisipate. Ukate, kwa nini uiharibu inchi pia? 8Akamjibu, akamwambia, Bwana, uache mwaka huu nao, hatta nikaupalilie, na kuusamadi: 9nao ukizaa matunda, vyema, la! haukuzaa, ndipo utaukata.
10Akawa akifundisha katika sunagogi mojawapo siku ya sabato. 11Na tazama, palikuwa na mwanamke aliyekuwa na pepo wa udhaifu miaka kumi na minane: nae amepindana, asiweze kujiinua kabisa. 12Bassi Yesu alipomwona, akamwita, akamwambia, Ee mwanamke, umefunguliwa udhaifu wako. 13Akaweka mikono yake juu yake, akanyoka marra hiyo, akaanza kumtukuza Mungu. 14Mkuu wa ile sunagogi akajibu, akiona hasira kwa sababu Yesu amemponya mtu siku ya sabato, akawaambia makutano, Kuna siku sita itupasapo kufauya kazi: katika hizo, bassi, njoni mponywe wala si katika siku ya sabato. 15Bassi Bwana akamjibu, akasema, Ewe mnafiki, killa mmoja wenu je! hamfungui ngʼombe wake au punda wake mazizini siku ya sabato, akaenda nae kumnywesha? 16Na huyu, aliye binti Ibrahimu, amhae Shetani amemfunga miaka kumi na minane hii, haikupasa afunguliwe kifungo hiki siku ya sabato? 17Na aliposema haya, watu wote walioshindana nae wakatahayarika, mkutano wote wakafurahi kwa ajili ya mambo matukufu yaliyotendwa nae.
18Bassi, akasema, Ufalme wa Mungu umefanana na nini? Na niufananishe na nini? 19Umefanana na punje ya kharadali, aliyotwaa mtu akaitupa katika shamba lake, ikakua, ikawa mti mkubwa, ndege za anga wakatua katika matawi yake. 20Akasema marra ya pili, Niufananishe na nini ufalme wa Mungu? 21Umefanana na chachu aliyotwaa mwanamke akaisetiri katika pishi tatu za unga, hatta ukachacha wote pia. 22Akawa akizungukazunguka katika miji ni vijiji, akifundisha, na kufanya safari kwenda Yerusalemi. 23Mtu mmoja akamwambia, Bwana, wao wanaookolewa ni wachaehe? 24Akawaambia, Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba; kwa maana nawaambieni ya kwamba watu wengi watatafuta kuingia nao bawataweza. 25Tokea wakati ule atakapoondoka mwenye nyumba na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkinena, Bwana, Bwana! utufungulie; nae akajibu, akawaambieni, Siwajui mtokako; 26ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula, na kunywa mbele yako; nawe ulifundisha kalika njia zetu; 27nae atasema, Nawaambieni, Siwajui mtokako: ondokeni mbali nami, ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu. 28Hapo kutakuwako kulia na kusaga meno, mtakapomwona Ibrahimu na Isaak na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, na ninyi wenyewe nikitupwa nje. 29Na watakuja watu toka maawio ya jua na machweo yake na toka kaskazini na kusini, nao wataketi katika ufalme wa Mungu. 30Kafahamuni, wako wa mwisho watakaokuwa wa kwanza, na wako wa kwanza watakaokuwa wa mwisho.
31Siku ile ile baadhi ya Mafarisayo wakamwendea, wakamwambia, Ondoka hapa, ukaende zako: kwa maana Herode anataka kukuua. 32Akawaambia, Enendeni zenu, nikamwambie yule mbweha, Tazama, nafukuza pepo, nafanya kazi ya kuwaponya watu leo na kesho, nami siku ya tatu nakamilika. 33Illakini imenipasa kushika njia yangu leo na kesho na kesho kutwa, kwa maana haimkini nabii aangamie nje ya Yerusalemi. 34Ee Yerusalemi, Yerusalemi, uwauae manabii na kuwapiga mawe wao waliotumwa kwako! marra ngapi nimetaka kuwakusanya watoto wako kama vile kuku avikusanyavyo vifaranga vyake chini ya mbawa zake, wala hanikutaka! 35Angalieni, nyumba yenu imeachwa ukiwa. Amin, nawaambieni, Hamtaniona kabisa hatta wakati ule mtakaposema, Amebarikiwa yeye ajae kwa jina la Bwana.

Iliyochaguliwa sasa

Luka MT. 13: SWZZB1921

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia