Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Luka MT. 1

1
1KWA kuwa wiitu wengi wametia mkono kutunga khabari za mambo yale yaliyotimizwa kati yetu, 2kama walivyotuhadithia wale waliokuwa mashahidi, ua watumishi wa lile neno tokea mwanzo, 3nimeona vema na mimi, nikiisha kujipatia khabari zilizo sahihi za mambo yote tokea awali, kukuandikia kwa taratibu. Theofilo il-aziz: 4upate kujua usahihi wa maneno yale uliyofundishwa.
5Zamani za Herode, mfalme wa Yahudi, palikuwa na kuliani mmoja, jina lake Zakaria, wa zamu ya Abiya: na mkewe alikuwa mmojawapo wa binti Haruni, jina lake Elizabeti. 6Nao wote wawili wenye haki mbele ya Mungu, wakiendelea katika amri zote za Bwana na hukumu zake zote bila lawama. 7Nao walikuwa hawana mtoto; maana Elizabeti alikuwa tassa, nao wote wawili wazec sana.
8Bassi ikawa alipokuwa akifanya kazi ya ukuhani katika taratibu ya zamu yake mbele ya Mungu, 9kama ilivyokuwa desturi ya ukubani, kura ikamwangukia kuingia katika hekalu la Bwana, na kufukiza uvumba. 10Na mkutano wote wa watu walikuwa wakisali nje, saa ya kufukiza. 11Akatokewa na Malaika wa Bwana, amesimama upande wa kuume wa madhbahu ya kufukizia. 12Zakaria akafadhaika alipomwona, khofu ikamwingia. 13Yule malaika akamwambia, Usiogope, Zakaria, maana dua yako imesikiwa, na mke wako Elizabeti atakuzalia mtoto mwanamume, na jina lake utamwita Yohana. 14Nawe utakuwa na furaha na shangwe; na watu wengi watafurahia kuzaliwa kwake. 15Kwa maani atakuwa mkuu mbele ya Mungu, hatakunywa divai wala kileo: nae atajazwa Roho Mtakatifu hatta tangu tumbo la mama yake. 16Na wengi katika wana wa Israeli atawarejeza kwa Bwana Mungu wao. 17Nae atatangulia mbele ya uso wake, mwenye roho ya Eliya, na nguvu zake, kuigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na kuwageuza maasi waelekee akili zao wenye haki; illi kumfanyia tayari Bwana watu waliotengenezwa. 18Zakaria akamwambia malaika, Nitajuaje hayo? Maana mimi mzee na mke wangu kongwe wa siku nyingi.
19Malaika akamjibu, akamwambia, Mimi ni Gabrieli nisimamae mbele ya Mungu: nami nalitumwa niseme nawe, na kukupasha khabari hizi njema. 20Nawe utakuwa bubu, usiweze kusema hatta siku ile yatakapotokea hayo: kwa sababu hukusadiki maneno yangu: nayo yatatimizwa wakati wake. 21Na wale watu walikuwa wakimugojea Zakaria, wakastaajabu kwa kukawia kwake mle hekaluni: 22hatta alipotoka hakuweza kusema nao, wakatambua ya kuwa ameona maono mle hekaluni; nae alikuwa akiwapungia mkouo, akadumu kuwa bubu. 23Ikawa siku za khuduma yake zilipotimia, akaenda zake nyumbani kwake.
24Hatta baada ya siku zile mkewe Elizabeti akachukua mimba akajificha miezi mitano, akisema, 25Hivi ndivyo alivyonitendea Bwana, siku zile alizoniangalia, kuniondolea aibu yangu mbele ya watu.
26Mwezi wa sita malaika Gabrieli alipelekwa na Mungu kwenda mji wa Galilaya, jina lake Nazareti, 27kwa mwanamke bikira aliyekuwa ameposwa na mume, jina lake Yusuf, wa nyumba ya Daud; na jina la yule mwanamke Mariamu. 28Akaja kwake akasema, Salamu, uliyepewa neema, Bwana yu pamoja nawe. 29Nae akafadhaika kwa khabari ya neno hili, akawaza moyoni mwake, Hii ni salamu gani? 30Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu; kwa maana umepata neema kwa Mungu. 31Tazama, utachukua mimba, utazaa mwana, utamwita jina lake Yesu. 32Huyu atakuwa mkuu, atakwitwa Mwana wake Aliye juu; na Bwana Mungu atampa kiti cha Daud baba yake. 33Ataimiliki nyumba ya Yakobo hatta milele; wala ufalme wake hautakuwa na mwisho. 34Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno hili; kwa maana simjui mume? 35Malaika akajibu, akamwambia, Roho Mtakatifu atakujia, na nguvu zake Aliye juu zitakutilia kivuli: kwa biyo kitakachozaliwa kitakwitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu. 36Na tazama, nae Elizabeti jamaa yako, ana mimba ya mtoto mume katika uzee wake: na mwezi hun wa sita kwake yeye aliyekwitwa tassa: 37kwa maana hapana neno lisilowezekana kwa Mungu. 38Mariamu akasema, Tazama, mimi mjakazi wa Bwana; na iwe kwangu kwa neno lako. Malaika akaondoka kwake.
39Mariamu akaondoka siku hizo, akaenda milimani kwa haraka hatta mji mmoja wa Yuda. 40Akaingia nyumbani kwa Zakaria, akamwamkia Elizabeti. 41Ikawa Elizabeti alipoisikia salamu ya Mariamu, mtoto mchanga akaruka ndani ya tumbo lake; Elizabeti akajazwa Roho Mtakatifu, akapaaza sauti yake kwa nguvu, akasema, 42Umebarikiwa wewe katika wanawake, na uzao wa tumbo lako umebarikiwa. 43Na latoka wapi neno hili lililonipata, mama wa Bwana wangu anijilie mimi? 44Kwa maana sauti ya salamu yako ilipoingia masikioni mwangu, mtoto mchanga aliruka kwa shangwe ndani ya tumbo langu. 45Na yu kheri aliyesadiki, kwa maana maneno hayo aliyoambiwa na Bwana yatatimizwa. 46Mariamu akasema,
Moyo wangu wamwadhimisha Bwana,
47Roho yangu yamfurahia Mungu, Mwokozi wangu.
48Kwa kuwa ameutazama unyonge wa mjakazi wake:
Kwa maana hakika, tokea leo vizazi vyote wataniita kheri.
49Kwa kuwa aliye hodari amenitendea makuu;
Na Jina lake ni takatifu.
50Na rehema zake vizazi hatta vizazi
Kwao wanaomcha.
51Ametenda nguvu kwa mkono wake;
Amewatawanya walio na kiburi katika mioyo yao.
52Amewashusha wakuu katika viti,
Amewakweza wanyonge.
53Wenye njaa amewashibisha mema;
Wenye mali amewaondoa mikono mitupu
54Kwa kukumbuka rehema
Amemsaidia Israeli mtumishi wake,
55(Kwa jinsi alivyowaambia baba zetu)
Ibrahimu na nzao wake, hatta milele.
56Mariamu akakaa nae kadri ya miezi mitatu, akarudi nyumbani kwake.
57Hatta Elisabeti akatimiziwa wakati wake wa kuzaa, akazaa mwana mume. 58Wakasikia jirani zake na jamaa zake ya kwamba Bwana amemwongezea rehema zake; wakafurahiwa pamoja nae. 59Ikawa siku ya nane wakaja kumtahiri mtoto; wakataka kumpa jina la babae, Zakaria. 60Akajibu mamae, akasema, Sivyo, lakini atakwitwa Yohana. 61Wakamwambia, Hapana mtu katika jamaa zako aitwae jina hilo. 62Wakamwashiria babae, kumwuliza atakaje aitwe. 63Akataka kibau, akaandika, akanena, Yohana ni jina lake. Wakataajabu wote. 64Marra akafunguliwa kinywa na ulimi wake, akanena, akimbariki Mungu. 65Khofu ikawaingia wote waliokaa karibu nao; yakaenea maneno haya pia milimani mwote Uyahudi. 66Na wote waliosikia wakayaweka mioyoni mwao, wakinena, Mtoto gani bassi atakuwa huyu? Kwa maana mkono wa Bwana ulikuwa pamoja nae? 67Zakaria babae akajazwa Roho Mtakatifu, akatabiri, akinena,
68Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli;
Kwa kuwa amewajia watu wake na kuwakomboa.
69Ametuondokeshea wokofu wa nguvu
Katika nyumba ya Daud mtumishi wake.
70(Kama alivyosema kwa vinywa vya manabii wake watakatifu tangu mwanzo),
71Tuokolewe na adui zetu, na katika mikono yao wote wauaotuchukia;
72Illi kuwatendea rehema baba zetu,
Na kukumbuka agano lake takatifu;
73Uapo aliomwapia Ibrahimu baba yetu,
74Ya kwamba atatupa sisi, tukiokoka mikononi mwa adui zetu,
tumwabudu pasipo khofu,
75Katika utakatifu na kwa haki mbele zake siku zetu zote.
76Na wewe nawe, Mtoto, utakwitwa nabii wake Aliye juu:
Kwa maana utatangulia mbele ya uso wake
Bwana ufanyize njia zake;
77Uwajulishe watu wake wokofu
Zikiondolewa dhambi zao,
78Kwa rehema zake Mungu wetu,
Kwazo mwangaza wa juu umetujia,
79Kuwaangaza wakaao katika giza na uvuli wa mauti,
Na kuelekeza miguu yetu mnamo njia ya amani.
80Yule mtoto akakua akaongezeka nguvu rohoni; akawako majangwani hatta siku ya kutokea kwake kwa Israeli.

Iliyochaguliwa sasa

Luka MT. 1: SWZZB1921

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia