Luka 18
18
Mfano wa mjanena hakimu
1Basi, Yesu aliwasimulia mfano kuonesha kwamba ni lazima kusali daima bila kukata tamaa.#18:1 Tazama Luka 11:5-8. Mifano hiyo miwili inaonesha upendeleo wa pekee wa Luka juu ya jambo muhimu la sala (Luka 3:21 maelezo). Na kuhusu kusali daima Ling na Luka 21:36. Jambo la kustahimili katika sala anafundisha pia Paulo (Rom 12:12; Kol 4:2; 1Thes 5:17). 2Alisema: “Katika mji mmoja kulikuwa na hakimu ambaye hakuwa anamcha Mungu wala kumjali binadamu. 3Katika mji huohuo, kulikuwa pia na mama mmoja mjane ambaye alimwendea huyo hakimu mara nyingi akimwomba amtetee apate haki yake kutoka kwa adui yake.#18:3,6 Mama mjane anaomba haki yake na kuamua kuifuatilia hata kama alikuwa dhaifu; huyo hakimu anaitwa “mbaya” (au mtovu wa haki) kwa kutomsikiliza huyo mama. 4Kwa muda mrefu huyo hakimu hakupenda kumtetea huyo mjane; lakini, mwishowe akajisemea: ‘Ingawa mimi simchi Mungu wala simjali binadamu, 5lakini kwa vile huyu mjane ananisumbua, nitamtetea; la sivyo ataendelea kufika hapa, na mwisho atanichosha kabisa!’”
6Basi, Bwana akaendelea kusema, “Sikieni jinsi alivyosema huyo hakimu mbaya. 7Je, ndio kusema Mungu hatawatetea wale aliowachagua, ambao wanamlilia mchana na usiku? Je, atakawia kuwasikiliza? 8Nawaambieni atawatetea upesi. Hata hivyo, je, kutakuwako na imani duniani wakati Mwana wa Mtu atakapokuja?”
Mfano wa Mfarisayona mtozaushuru
9Halafu Yesu aliwaambia pia mfano wale ambao walijiona kuwa wema na kuwadharau wengine.#18:9 Kuwa na uhusiano mwema na Mungu kunapatikana kwa kuachana na dhambi na kumgeukia Mungu (15:7,10) wala siyo kwa kumweleza Mungu mema uliyofanya. 10“Watu wawili walipanda kwenda hekaluni kusali:#18:10 Kusali: Sala ya hadhara ilifanyika hekaluni asubuhi na jioni nyakati zilizowekwa; lakini sala ya faragha au binafsi ilifanyika wakati wowote ule. mmoja Mfarisayo, na mwingine mtozaushuru. 11Huyo Mfarisayo#18:11 Mfarisayo: Mmoja wa wale ambao walijidhania kuwa waaminifu katika kutekeleza matakwa yao ya kidini kuliko wengine. Tazama pia Orodha ya Maneno. akasimama, akasali kimoyomoyo:#18:11 Akasali kimoyomoyo: Neno kwa neno: akasali kwake, au: akasali naye mwenyewe, au: bila sauti ndogo. Ling na Mat 6:5. ‘Ee Mungu, nakushukuru kwa vile mimi si kama watu wengine: walafi, wadanganyifu au wazinzi. Nakushukuru kwamba mimi si kama huyu mtozaushuru.#18:11 Mtozaushuru: Watozaushuru walifikiriwa na watu wengine kuwa “wenye dhambi”. 12Nafunga mara mbili kwa juma, natoa zaka sehemu ya kumi ya pato langu.’ 13Lakini yule mtozaushuru, akiwa amesimama kwa mbali bila hata kuinua macho yake mbinguni, ila tu akijipiga kifua#18:13 Akijipiga kifua: Ishara ya masikitiko na toba (Luka 23:48). kwa huzuni, alisema: ‘Ee Mungu, unionee huruma#18:13 Unionee huruma: Ling na Zab 51:1. mimi mwenye dhambi.’ 14Nawaambieni, huyu mtozaushuru alirudi nyumbani akiwa amesamehewa.#18:14 Amesamehewa: Maana yake amesamehewa na Mungu, amepatanishwa naye au: amefanywa mwadilifu. Lakini yule mwingine, sivyo. Kwa maana kila anayejikweza atashushwa, na kila anayejishusha atakwezwa.”
Yesu anawabariki watoto wadogo
(Mat 19:13-15; Marko 10:13-16)
15Watu walimletea Yesu watoto wadogo ili awawekee mikono yake. Wanafunzi walipowaona, wakawazuia kwa maneno makali. 16Lakini Yesu akawaita kwake akisema: “Waacheni hao watoto waje kwangu, wala msiwazuie, kwa maana ufalme wa Mungu ni kwa ajili ya watu kama hawa. 17Nawaambieni kweli, mtu yeyote asiyeupokea ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo, hataingia katika ufalme huo.”
Tajiri mmoja#18:18-30 Njia ya uhai wa milele yafikiwa sio kwa kutekeleza yote yanayotakiwa na sheria ila kwa kujiacha kabisa mikononi mwa Mungu kwa kumfuata Yesu. Huu ndio ujumbe wa kisa hiki kulingana na (aya 30) ambayo ni jibu kamili sio tu kwa swali la Petro (aya 28) bali pia kama jibu kamilifu zaidi kwa swali la huyo kiongozi wa Wayahudi (aya 18).
(Mat 19:16-30; Marko 10:17-31)
18Kiongozi mmoja,#18:18 Kiongozi mmoja: Yaani, mmoja wa wakuu wa Wayahudi. Myahudi, alimwuliza Yesu, “Mwalimu mwema, nifanye nini ili niweze kuupata uhai wa milele?” 19Yesu akamwambia, “Mbona waniita mwema? Hakuna aliye mwema ila Mungu peke yake. 20Unazijua amri: ‘Usizini; Usiue; Usiibe; Usitoe ushahidi wa uongo; Waheshimu baba yako na mama yako.’”#18:20 Taz Kut 20:12-16; Kumb 5:16-20. Yesu anakariri amri tano tu za Amri Kumi. 21Yeye akasema, “Hayo yote nimeyazingatia tangu ujana wangu.”#18:21 Tangu ujana wangu: Yapata umri wa miaka kumi na miwili, umri ambao mtoto alichukuliwa kuwa ameanza kuwajibika kidini (2:42). 22Yesu aliposikia hayo, akamwambia, “Unatakiwa bado kufanya kitu kimoja: uza kila kitu ulicho nacho, wagawie maskini hiyo fedha, nawe utakuwa na hazina yako mbinguni; halafu njoo unifuate.” 23Lakini huyo mtu aliposikia hayo, alihuzunika sana kwa sababu alikuwa tajiri sana.
24Yesu alipoona akihuzunika hivyo, akasema, “Jinsi gani ilivyo vigumu kwa matajiri kuingia katika ufalme wa Mungu! 25Naam, ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano,#18:25 Ngamia kupita katika tundu la sindano: Msemo wenye shabaha ya kuonesha jambo lisilowezekana na ndivyo wanavyoelewa wafuasi wake (aya 26). Lakini (aya 27) Mungu anaweza kufanya kile ambacho kwa binadamu hakiwezekani. kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.” 26Wale watu waliposikia hayo, wakasema, “Nani basi, atakayeokolewa?” 27Yesu akajibu, “Yasiyowezekana kwa binadamu, yanawezekana kwa Mungu.”
28Naye Petro akamwuliza, “Na sisi, je? Tumeacha vitu vyote tukakufuata!” 29Yesu akawaambia, “Kweli nawaambieni, mtu yeyote aliyeacha nyumba au mke au ndugu au wazazi au watoto kwa ajili ya ufalme wa Mungu, 30atapokea mengi zaidi wakati huu wa sasa, na uhai wa milele wakati ujao.”
Yesu anasema mara ya tatu kuhusu kifo na ufufuo wake
(Mat 20:17-19; Marko 10:32-34)
31Yesu aliwachukua kando wale kumi na wawili, akawaambia, “Sikilizeni! Tunakwenda Yerusalemu#18:31 Tunakwenda Yerusalemu: Taz Luka 9:51—19:27 maelezo. na huko kila kitu kilichoandikwa na manabii kuhusu Mwana wa Mtu kitakamilishwa. 32Kwa maana atakabidhiwa kwa watu wa mataifa#18:32 Watu wa mataifa: Yaani, watawala wa Waroma. nao watamtendea vibaya na kumtemea mate. 33Watampiga mijeledi na kumuua; lakini siku ya tatu atafufuka.” 34Lakini wao hawakuelewa jambo hilo hata kidogo; walikuwa wamefichwa maana ya maneno hayo, na hawakutambua yaliyosemwa.
Yesu anamponya kipofu
(Mat 20:29-34; Marko 10:46-52)
35Wakati Yesu alipokaribia Yeriko, kulikuwa na mtu mmoja kipofu ameketi njiani akiomba. 36Aliposikia umati wa watu ukipita aliuliza, “Kuna nini?” 37Wakamwambia, “Yesu wa Nazareti anapita.” 38Naye akapaza sauti akisema, “Yesu, Mwana wa Daudi,#18:38 Mwana wa Daudi: Jina la kimasiha. Jina la kumtaja Masiha, yaani yule aliyetumwa na Mungu kuwaokoa watu wake. nihurumie!” 39Wale watu waliotangulia wakamkemea wakimwambia anyamaze; lakini yeye akazidi kupaza sauti: “Mwana wa Daudi, nihurumie!” 40Yesu alisimama, akaamuru wamlete mbele yake. Yule kipofu alipofika karibu, Yesu akamwuliza, 41“Unataka nikufanyie nini?” Naye akamjibu, “Bwana, naomba nipate kuona.” 42Yesu akamwambia, “Ona! Imani yako imekuponya.” 43Na mara huyo kipofu akapata kuona, akamfuata Yesu akimtukuza Mungu. Watu wote walipoona hayo, wakamsifu Mungu.
Iliyochaguliwa sasa
Luka 18: BHNTLK
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Copyright The Bible Society of Tanzania, 1993
The Bible Society of Kenya 1993