Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yohane 18

18
Yesu anatiwa nguvuni
(Mat 26:47-56; Marko 14:43-50; Luka 22:47-53)
1Yesu alipokwisha sema hayo, alikwenda ng'ambo ya kijito Kedroni,#18:1 Kedroni: Ni kijito ambacho kilitenga Yerusalemu na eneo la Mlima wa Mizeituni. Karibu na tambarare ya mlima huo kulikuwa na bustani (inaitwa Bustani ya Gethsemane katika zile Injili nyingine). Nabii Zekaria (14:1-4) anasema kwamba Mungu atatokea katika mlima huo na kuwashinda maadui zake. pamoja na wanafunzi wake. Mahali hapo palikuwa na bustani, naye Yesu akaingia humo pamoja na wanafunzi wake. 2Yuda, aliyemsaliti Yesu, alipajua mahali hapo kwani mara nyingi Yesu alikutana na wanafunzi wake huko. 3Basi, Yuda alichukua kikosi cha askari na walinzi#18:3 Kikosi cha askari na walinzi: Askari wa Roma walikuwa wamewekwa huko karibu na ngome ya Antonia na walikuwa na wajibu wa kudhibiti amani. Huenda Mafarisayo na viongozi wa Wayahudi walikuwa wamewaambia askari hao wamkamate Yesu kwa kuwaambia kwamba alikuwa mwasi hatari. kutoka kwa makuhani wakuu#18:3 Makuhani wakuu: Yaani Anasi na Kayafa (taz pia Luka 3:2). na Mafarisayo, akaja nao bustanini wakiwa na taa, mienge na silaha. 4Yesu, hali akijua yote yatakayompata, akatokea, akawauliza, “Mnamtafuta nani?” 5Nao wakamjibu, “Yesu Mnazareti!”#18:5 Yesu Mnazareti: Ilikuwa kawaida kumtambulisha mtu kwa kutaja mahali alikotoka. Yesu akawaambia, “Mimi ndiye.”#18:5 Mimi ndiye: Au “Mimi ndimi”. Tazama maelezo ya 8:24. Msaliti Yuda alikuwa amesimama hapo pamoja nao.
6Basi, Yesu alipowaambia: “Mimi ndiye,” wakarudi nyuma, wakaanguka chini. 7Yesu akawauliza tena, “Mnamtafuta nani?” Wakamjibu, “Yesu Mnazareti!” 8Yesu akawaambia, “Nimekwisha waambieni kwamba mimi ndiye. Basi, kama mnanitafuta mimi, waacheni hawa waende zao.” ( 9Alisema hayo ili yapate kutimia yale aliyosema: “Wale ulionipa sikumpoteza hata mmoja.”) 10Simoni Petro alikuwa na upanga; basi, akauchomoa, akamkata sikio la kulia mtumishi wa kuhani mkuu. Mtumishi huyo aliitwa Malko.#18:10 Injili zote nne zinaeleza tukio hili lakini ni Injili hii ya nne tu inataja majina ya wahusika yaani, Simoni Petro na Malko. 11Basi, Yesu akamwambia Petro, “Rudisha upanga wako alani. Je, nisinywe kikombe cha mateso#18:11 Kikombe cha mateso: Katika Biblia mara nyingine kikombe kinatumiwa kama mfano wa mateso, na maneno kunywa kikombe ni kuteseka (taz 4:34 maelezo). alichonipa Baba?”
Yesu mbele ya Kuhani Mkuu
12Kile kikosi cha askari, mkuu wake na walinzi wa Wayahudi walimkamata Yesu, wakamfunga 13na kumpeleka kwanza kwa Anasi;#18:13 Anasi: Huyu alikuwa kuhani mkuu Yesu alipokuwa kijana lakini wanawe na mkwe wake aitwaya Kayafa walifanywa kuwa makuhani na Waroma baada ya yeye Anasi kulazimishwa kuacha madaraka ya kuhani mkuu. Hata hivyo Anasi aliendelea kushikilia wadhifa huo kwa jina tu na mara nyingine walimwendea kutaka ushauri kwake. Anasi alikuwa baba mkwe wa Kayafa ambaye alikuwa kuhani mkuu mwaka huo. 14Huyo Kayafa ndiye aliyekuwa amewashauri Wayahudi kwamba ni afadhali mtu mmoja afe kwa ajili ya watu.
Petro anamkana Yesu
(Mat 26:69-70; Marko 14:66-68; Luka 22:55-57)
15Simoni Petro pamoja na mwanafunzi mwingine#18:15 Simoni Petro pamoja na mwanafunzi mwingine: Jina la mwanafunzi huyo halitajwi, lakini yafikiriwa ya kwamba alikuwa yule aliyependwa na Yesu (taz 13:23), aliyekuwa pale msalabani (19:25-27) na ambaye alikwenda na Petro kule kaburini baada ya Yesu kufufuka (20:1-10). walimfuata Yesu. Huyo mwanafunzi mwingine alikuwa anajulikana kwa kuhani mkuu, hivyo aliingia pamoja na Yesu ndani ya ukumbi wa kuhani mkuu. 16Lakini Petro alikuwa amesimama nje, karibu na mlango. Basi, huyo mwanafunzi mwingine aliyekuwa anajulikana kwa kuhani mkuu alitoka nje akasema na mjakazi, mngojamlango, akamwingiza Petro ndani. 17Huyo mjakazi mngojamlango akamwuliza Petro, “Je, nawe pia ni mmoja wa wanafunzi wa mtu huyu?” Petro akamwambia, “Si mimi!”
18Watumishi na walinzi walikuwa wamewasha moto kwa sababu kulikuwa na baridi, wakawa wanaota moto. Naye Petro alikuwa amesimama pamoja nao akiota moto.
Kuhani mkuu anamhoji Yesu
(Mat 26:59-66; Marko 14:55-64; Luka 22:66-71)
19Basi, kuhani mkuu#18:19 Kuhani mkuu: Yaani Anasi (aya 13,24). Kadiri ya Injili zile nyingine Yesu alipelekwa kuhukumiwa mbele ya kuhani mkuu na baraza la Wayahudi (Mat 26:57-68; Marko 14:55-65; Luka 22:66-71). akamwuliza Yesu juu ya wanafunzi wake na mafundisho yake. 20Yesu akamjibu, “Nimesema na kila mtu daima hadharani. Kila mara nimefundisha katika masunagogi na hekaluni, mahali wanapokutana Wayahudi wote; na wala sijasema chochote kwa siri. 21Kwa nini waniuliza mimi?#18:21 Kwa nini waniuliza mimi?: Hoja ya Yesu (aya 20-21) inaeleweka kulingana na taratibu za mahakama wakati huo. Yesu anawataka kesi iendeshwe kisheria pamoja na mashahidi. Waulize wale waliosikia nini niliwaambia. Wao wanajua niliyowaambia.” 22Alipokwisha sema hayo mlinzi mmoja aliyekuwa amesimama hapo akampiga kofi akisema, “Je, ndivyo unavyomjibu kuhani mkuu?” 23Yesu akamjibu, “Kama nimesema vibaya, onesha huo ubaya; lakini ikiwa nimesema vema, mbona wanipiga?” 24Basi, Anasi akampeleka Yesu akiwa amefungwa, kwa kuhani mkuu Kayafa.
Petro anamkana Yesu tena
(Mat 26:71-75; Marko 14:69-72; Luka 22:58-62)
25Petro alikuwa hapo akiota moto. Basi, wakamwuliza, “Je, nawe pia si mmoja wa wanafunzi wake?” Yeye akakana na kusema, “Si mimi!” 26Mmoja wa watumishi wa kuhani mkuu, jamaa wa yule aliyekatwa sikio na Petro, akamwuliza, “Je, mimi sikukuona wewe bustanini pamoja naye?” 27Petro akakana tena; mara jogoo akawika.
Yesu mbele ya Pilato
(Mat 27:1-2,11-14; Marko 15:1-5; Luka 23:1-5)
28Basi, walimchukua Yesu kutoka kwa Kayafa, wakampeleka ikulu. Ilikuwa alfajiri, nao ili waweze kula Pasaka, hawakuingia ndani ya ikulu wasije wakatiwa unajisi. 29Kwa hiyo, Pilato#18:29 Pilato: Ndiye aliyekuwa gavana wa mkoa wa Yudea, Samaria na Idumea; alikuwa na wadhifa huo tangu 26 B.K. mpaka 36 B.K. Aliishi Kaisarea lakini alikwenda Yerusalemu wakati wa sikukuu kubwa kama hiyo ya Pasaka. aliwaendea nje, akasema, “Mna mashtaka gani juu ya mtu huyu?” 30Wakamjibu, “Kama huyu hangalikuwa mwovu hatungalimleta kwako.” 31Pilato akawaambia, “Haya, mchukueni nyinyi wenyewe, mkamhukumu kufuatana na sheria yenu.” Wayahudi wakamjibu, “Sisi hatuna mamlaka ya kumwua mtu yeyote.”#18:31 Hatuna mamlaka ya kumwua mtu yeyote: Inawezekana kwamba wakuu wa Roma hawakuwaruhusu Wayahudi kumuua mtu yeyote isipokuwa kama imedhihirika wazi kabisa kwamba alikuwa na hatia. ( 32Ilifanyika hivyo yapate kutimia maneno aliyosema Yesu kuonesha atakufa kifo gani.)#18:32 Aliyosema Yesu kuonesha atakufa kifo gani: Yaani kifo juu ya msalaba. Namna hiyo ya kuuawa haikuwa katika sheria ya Wayahudi. Waroma walitoa hukumu ya namna hiyo kwa wote ambao hawakuwa wananchi wa Roma, na hukumu hiyo ilitolewa kwa kuadhibu visa vikubwa kama vile maasi. 33Pilato akaingia tena ndani ya ikulu, akamwita Yesu na kumwuliza: “Ati wewe ndiye Mfalme wa Wayahudi?”#18:33 Ati wewe ndiye mfalme wa Wayahudi?: Kama Yesu angekubali kuwa ni mfalme wa kweli angaliweza kuhukumiwa kama mwasi wa siasa. Uasi dhidi ya mfalme mkuu wa Roma uliadhibiwa kwa kusulubiwa msalabani. Taz Mat 27:11. 34Yesu akamjibu, “Je, hayo ni maneno yako au wengine wamekuambia habari zangu?” 35Pilato akamjibu, “Je, ni Myahudi mimi? Taifa lako na makuhani wamekuleta kwangu. Umefanya nini?” 36Yesu akamjibu, “Ufalme wangu si wa ulimwengu huu.#18:36 Ufalme wangu si wa ulimwengu huu: Taz 3:3. Kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu, watumishi wangu wangenipigania nisitiwe mikononi mwa Wayahudi. Lakini sasa ufalme wangu si wa hapa.” 37Hapo Pilato akamwambia, “Basi, wewe ni Mfalme?” Yesu akajibu, “Wewe umesema kwamba mimi ni Mfalme. Mimi nimezaliwa kwa ajili hiyo; na kwa ajili hiyo nimekuja ulimwenguni kuwaambia watu juu ya ukweli. Kila mtu wa ukweli hunisikiliza.” 38Pilato akamwambia, “Ukweli ni kitu gani?”
Yesu anahukumiwa kufa
(Mat 27:15-31; Marko 15:6-20; Luka 23:13-25)
Pilato alipokwisha sema hayo, aliwaendea tena Wayahudi nje, akawaambia, “Mimi sioni hatia yoyote kwake. 39Lakini, mnayo desturi kwamba mimi niwafungulie mfungwa mmoja wakati wa Pasaka.#18:39 Desturi …niwafungulie mfungwa mmoja wakati wa Pasaka: Taz pia Mat 27:15; Marko 15:6. Hatuna mahali pengine ambapo desturi hiyo inatajwa au kuelezwa. Basi, mwataka niwafungulieni Mfalme wa Wayahudi?” 40Hapo wakapiga kelele: “La! Si huyu ila Baraba!”#18:40 Baraba: Luka (23:19) anajazia kwamba alikuwa mtu aliyetiwa ndani kwa kusababisha uasi na mauaji. Hakuna habari zaidi kuhusu maisha yake. Naye Baraba alikuwa mnyang'anyi.

Iliyochaguliwa sasa

Yohane 18: BHNTLK

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia