Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yohane 14

14
Yesu njia ya kwenda kwa Baba
1Yesu aliwaambia, “Msifadhaike mioyoni mwenu. Mwaminini Mungu, niaminini na mimi pia. 2Nyumbani mwa Baba yangu#14:2 Nyumbani mwa Baba yangu: Yesu anaongea hapa juu ya mbinguni. Taz pia Orodha ya Maneno. mna makao mengi; kama isingekuwa hivyo, ningalikwisha waambieni. Sasa nakwenda kuwatayarishieni nafasi. 3Na nikienda na kuwatayarishieni nafasi, nitarudi na kuwachukueni kwangu, ili nanyi muwe pale nilipo mimi. 4Mnajua njia ya kwenda huko ninakokwenda.”
5Thoma#14:5 Thoma: Mmoja wa wanafunzi 12 (taz Mat 10:3). Anaitwa pia Pacha, neno ambalo ni tafsiri ya Thoma kutokana na Kiaramu. Picha inayotolewa katika Injili ya Yohane ni kwamba huyu Thoma alikuwa mtu wa mashakamashaka (taz pia 20:24-29). akamwuliza, “Bwana, hatujui unakokwenda, tutawezaje basi, kuijua hiyo njia?” 6Yesu akamjibu, “Mimi ni njia, na ukweli na uhai.#14:6 Mimi ni njia, na ukweli na uhai: Yesu ni njia ya kwenda kwa Mungu; yeye ni ukweli wote juu ya Mungu na matakwa yake kuhusu binadamu; yeye ni uhai (rejea Yoh 1:4; 3:16; 11:25; 17:3; taz pia Yoh 6:35). Binadamu ataweza kwenda kwa Mungu Baba kwa kupitia kwa Yesu Kristo peke yake (Mat 11:27; Yoh 1:18; 6:46; Mate 4:12). Hakuna awezaye kwenda kwa Baba ila kwa kupitia kwangu. 7Ikiwa mnanijua mimi, mnamjua na Baba yangu pia. Na tangu sasa, mnamjua, tena mmekwisha mwona.”
8Filipo akamwambia, “Bwana, tuoneshe Baba, nasi tutatosheka.” 9Yesu akamwambia, “Nimekaa nanyi muda wote huu, nawe Filipo hujanijua? Aliyekwisha niona mimi amemwona Baba. Unawezaje basi, kusema: ‘Tuoneshe Baba?’ 10Je, huamini kwamba mimi niko ndani ya Baba, naye Baba yuko ndani yangu? Maneno ninayowaambieni siyasemi kwa mamlaka yangu; Baba aliye ndani yangu anafanya kazi yake. 11Mnapaswa kuniamini ninaposema kwamba mimi niko ndani ya Baba naye Baba yuko ndani yangu. Ama sivyo, aminini kwa sababu ya mambo ninayofanya. 12Kweli nawaambieni, anayeniamini atafanya mambo ninayofanya mimi; naam, atafanya hata makuu zaidi,#14:12 Atafanya hata makuu zaidi: Yesu anaporudi kwa Baba (7:33; 13:1; 14:28) atawajalia wafuasi wake uwezo wote wa Roho wa Mungu (7:39), ambao utawawezesha kutenda makuu zaidi hata kuliko yeye! kwani ninakwenda kwa Baba. 13Na chochote mtakachoomba kwa jina langu nitafanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. 14Mkiniomba chochote kwa jina langu, nitawafanyieni.
Roho Mtakatifu#14:15-26 Roho Mtakatifu: Roho Mtakatifu katika Biblia anaonekana tangu mwanzo kuhusika katika kazi ya Mungu ya kuumba ulimwengu (Mwa 1:2) akivipa viumbe (mimea, wanyama na watu) uhai (Zab 104:27-30). Kwa kuja kwake Yesu, Mwana wa Mungu, Roho huyo huyo wa Mungu ataendelea na kazi ya Yesu na atakaa na wafuasi wake (aya 16, 17), atawafundisha (aya 26), atamshuhudia kwao (15:26), atauhukumu ulimwengu usioamini (16:8-11).
15“Mkinipenda mtazishika amri zangu. 16Nami nitamwomba Baba naye atawapeni #14:16 Msaidizi: Neno lililotafsiriwa hapa kama Msaidizi ni “parakletos” katika Kigiriki nalo laweza pia kuwa na maana ya “mwombezi” (taz 1Yoh 2:1) au “wakili”. Roho Mtakatifu atachukua nafasi ya Yesu mwenyewe kama kiongozi na mwalimu wa wanafunzi wake (taz pia 14:26; 15:26; 16:7).Msaidizi#14:16-17 Msaidizi: Hapa inasemwa Msaidizi mwingine, yaani Yesu naye pia ni Msaidizi au Mwombezi au Mtetezi (taz 1Yoh 2:1 ambapo Yesu anaitwa moja kwa moja kwa jina hilo la Kigiriki “parakletos” yaani, Mwombezi, Mtetezi au Wakili, Msaidizi). mwingine, atakayekaa nanyi milele. 17Yeye ni Roho wa ukweli. Ulimwengu#14:17 Ulimwengu: Taz 12:31 maelezo. hauwezi kumpokea kwa sababu hauwezi kumwona wala kumjua. Lakini nyinyi mnamjua kwa sababu anabaki nanyi na yu ndani yenu.
18“Sitawaacha nyinyi yatima; nitakuja tena kwenu. 19Bado kidogo nao ulimwengu hautaniona tena, lakini nyinyi mtaniona; na kwa kuwa mimi ni hai, nanyi pia mtakuwa hai. 20Siku ile itakapofika mtajua kwamba mimi niko ndani ya Baba, nanyi mko ndani yangu, nami ndani yenu. 21Azipokeaye amri zangu na kuzishika, yeye ndiye anipendaye. Naye anipendaye mimi atapendwa na Baba yangu, nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.”
22Yuda#14:22 Yuda: Huenda ni sawa na Yuda mwana wa Yakobo anayetajwa katika Luka 6:16; Mate 1:13. (si yule Iskarioti) akamwambia, “Bwana, itawezekanaje wewe kujidhihirisha kwetu na si kwa ulimwengu?” 23Yesu akamjibu, “Mtu akinipenda atashika neno langu, na Baba yangu atampenda, nasi tutakuja kwake na kukaa naye. 24Asiyenipenda hashiki maneno yangu. Na neno mlilosikia si langu, bali ni lake Baba aliyenituma.
25“Nimewaambieni mambo haya nikiwa bado pamoja nanyi, 26lakini Msaidizi, Roho Mtakatifu, ambaye Baba atamtuma kwa jina langu, atawafundisheni kila kitu na kuwakumbusheni yote niliyowaambieni.
27“Nawaachieni amani;#14:27 Amani: Amani ambayo Yesu anawapa wanafunzi wake ni zaidi ya hali isiyo na misukosuko ya ndani na nje. Amani hiyo ni hali njema kamilifu ya roho na mwili. nawapeni amani yangu. Siwapi nyinyi kama vile ulimwengu ufanyavyo. Msiwe na wasiwasi, wala msifadhaike. 28Mlikwisha sikia nikiwaambieni: ‘Ninakwenda zangu, kisha nitarudi tena kwenu.’ Kama mngalinipenda, mngalifurahi kwa sababu ninakwenda kwa Baba, maana yeye ni mkuu kuliko mimi. 29Nimewaambieni haya sasa kabla hayajatokea, ili yatakapotokea mpate kuamini. 30Sitasema nanyi tena mambo mengi, maana mtawala wa ulimwengu huu#14:30 Mtawala wa ulimwengu huu: Yaani Shetani (taz 12:31 maelezo; 13:2,26,27; 16:11; Ufu 20:2-3,7-10). anakuja. Kwangu mimi hawezi kitu; 31lakini ulimwengu unapaswa kujua kwamba nampenda Baba, na ndiyo maana nafanya kila kitu kama Baba alivyoniamuru. Simameni, tutoke hapa!

Iliyochaguliwa sasa

Yohane 14: BHNTLK

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia