Yohane 13
13
Yesu anawaosha mitume miguu
1Ilikuwa siku kabla ya sikukuu ya Pasaka.#13:1 Kabla ya sikukuu ya Pasaka: Pasaka itaadhimishwa kesho yake, Ijumaa, wakati wa machweo ya jua. Katika Yohane Yesu alisulubiwa wakati kondoo wa Pasaka walipokuwa wanachinjwa. Yesu alijua kwamba saa yake ya kuondoka ulimwenguni na kwenda kwa Baba ilikuwa imefika. Alikuwa amewapenda daima watu wake walioko duniani; naam, aliwapenda mpaka mwisho!
2Basi, Yesu na wanafunzi wake walikuwa wamekaa kula chakula cha jioni. Ibilisi alikwisha mtia Yuda, mwana wa Simoni Iskarioti, nia ya kumsaliti Yesu.#13:2-11 Yesu anawaosha wanafunzi wake miguu: Katika utamaduni wa Wayahudi mgeni alipaswa kuosha miguu (taz Mwa 18:4; Luka 7:44); lakini hakuna habari kuhusu watu kuoshana miguu. Mtumwa wakati fulani aliweza kuosha miguu ya bwana wake. Kitendo cha Yesu hapa kinaashiria kitendo kikuu cha utumishi wake kitakachofanyika kwa kufa msalabani kwa ajili ya dhambi za ulimwengu. 3Yesu alijua kwamba Baba alikuwa amemkabidhi kila kitu, na kwamba alikuwa ametoka kwa Mungu na anarudi kwa Mungu. 4Basi, aliondoka mezani, akaweka kando vazi lake, akachukua kitambaa na kujifunga kiunoni. 5Kisha akatia maji katika bakuli, akaanza kuwaosha wanafunzi wake miguu na kuipangusa kwa kile kitambaa alichojifungia. 6Basi, akamfikia Simoni Petro; naye Petro akasema, “Bwana, wewe utaniosha miguu mimi?” 7Yesu akamjibu, “Huelewi sasa ninachofanya lakini utaelewa baadaye.”#13:7 Utaelewa baadaye: Ni baada ya kifo na ufufuo wake ndipo hao wanafunzi watakapoelewa kikamilifu mafundisho na matendo ya Yesu (2:22; 12:16; 16:4). 8Petro akamwambia, “Wewe hutaniosha miguu kamwe!” Yesu akamjibu, “Nisipokuosha hutakuwa na uhusiano nami tena.” 9Simoni Petro akamjibu, “Bwana, nioshe, si miguu tu, bali na mikono yangu na kichwa pia.” 10Yesu akamwambia, “Aliyekwisha oga hana lazima ya kunawa isipokuwa miguu, maana amekwisha takata mwili wote. Nyinyi mmetakata, lakini si nyote.” ( 11Yesu alimjua yule ambaye atamsaliti, ndiyo maana alisema: “Nyinyi mmetakata, lakini si nyote.”)#13:11 Mmetakata, lakini si nyote: Yesu alikuwa anamaanisha Yuda (13:2).
12Alipokwisha waosha miguu na kuvaa tena vazi lake, aliketi mezani, akawaambia, “Je, mmeelewa hayo niliyowatendeeni? 13Nyinyi mwaniita Mwalimu na Bwana,#13:13 Bwana: Neno la Kigiriki hapa ni “Kurios” na linapotumiwa kwa Yesu linachukua maana ya ukuu, uwezo na nguvu. nanyi mwasema vyema, kwa kuwa ndimi. 14Basi, ikiwa mimi niliye Bwana na Mwalimu nimewaosha nyinyi miguu, nanyi pia mnapaswa kuoshana miguu.#13:14 Mnapaswa kuoshana miguu: Bila shaka yahusu mfano wa unyenyekevu na huduma ya kindugu (1Tim 5:10). 15Nimewapeni mfano, ili nanyi pia mfanye kama nilivyowafanyieni. 16Kweli nawaambieni, mtumishi si mkuu kuliko bwana wake, wala mtume si mkuu kuliko yule aliyemtuma. 17Basi, ikiwa mwayajua hayo, mtakuwa na heri mkiyatekeleza.
18“Haya nisemayo hayawahusu nyinyi nyote. Mimi nawajua wale niliowachagua. Lakini lazima yatimie Maandiko Matakatifu yasemayo: ‘Yule aliyeshiriki chakula changu amegeuka kunishambulia.’ 19Mimi nimewaambieni mambo haya sasa kabla hayajatokea, ili yatakapotokea mpate kuamini kuwa ‘Mimi Ndimi.’#13:19 Mimi ndimi: Taz 8:24 maelezo. 20Kweli nawaambieni: anayempokea yule ninayemtuma ananipokea mimi; na anayenipokea mimi, anampokea yule aliyenituma.”
Yesu anabashiri kwamba atasalitiwa
(Mat 26:20-25; Marko 14:17-21; Luka 22:21-23)
21Alipokwisha sema hayo, Yesu alifadhaika sana rohoni, akasema wazi, “Kweli nawaambieni, mmoja wenu atanisaliti!” 22Wanafunzi wakatazamana wasiweze kabisa kujua anamsema nani. 23Mmoja wa wanafunzi, ambaye Yesu alikuwa anampenda sana,#13:23 Mmoja wa wanafunzi …Yesu alikuwa anampenda sana: Huyo anatajwa pia katika 19:26-27; 20:2-10; 21:7,20-24. Mapokeo ya kale yanamtambua kuwa ni mtume Yohane, mwana wa Zebedayo ambaye hatajwi kwa jina katika Injili hii. alikuwa ameketi karibu na Yesu. 24Basi, Simoni Petro akamwashiria na kusema: “Mwulize anasema juu ya nani.” 25Mwanafunzi huyo akasogea karibu zaidi na Yesu, akamwuliza, “Bwana, ni nani?” 26Yesu akajibu, “Yule nitakayempa kipande cha mkate nilichochovya katika sahani, ndiye.” Basi, akatwaa kipande cha mkate, akakichovya katika sahani, akampa Yuda, mwana wa Simoni Iskarioti. 27Yuda alipokwisha pokea kipande hicho, Shetani akamwingia.#13:27 Shetani akamwingia: Taz pia 13:2. Hapa mwandishi anataka kusema kwamba Shetani anamdhibiti Yuda kabisa. Basi Yesu akamwambia, “Unachotaka kufanya, kifanye haraka!” 28Lakini hakuna hata mmoja wa wale waliokaa pale mezani aliyefahamu kwa nini alikuwa amemwambia hivyo. 29Kwa kuwa Yuda alikuwa mweka hazina, baadhi yao walidhani kwamba Yesu alikuwa amemwambia anunue vilivyohitajiwa kwa sikukuu, au kwamba alikuwa amemwambia akatoe chochote kwa maskini. 30Basi, Yuda alipokwisha twaa kile kipande cha mkate, akatoka nje mara. Na ilikuwa usiku.#13:30 Ilikuwa usiku: Giza limekumba sio tu nchi bali pia roho yake Yuda mwenyewe (taz 9:4; 12:35).
Amri mpya
31Baada ya Yuda kuondoka, Yesu akasema, “Sasa#13:31 Sasa …: Wakati ule maalumu wa kufunuliwa kwa utukufu wa Yesu umefika. Mwana wa Mtu ametukuzwa, naye Mungu ametukuzwa ndani yake. 32Na kama utukufu wa Mungu umefunuliwa ndani ya Mwana, basi, naye Mungu ataudhihirisha utukufu wa Mwana ndani yake mwenyewe, na atafanya hivyo mara.
33“Watoto wangu, bado niko nanyi kwa muda mfupi tu. Mtanitafuta, lakini sasa nawaambieni yale niliyowaambia viongozi wa Wayahudi: ‘Niendako nyinyi hamwezi kwenda!’ 34Nawapeni amri mpya: pendaneni; pendaneni kama nilivyowapenda nyinyi.#13:34 Amri mpya: pendaneni kama nilivyowapenda nyinyi: Mapendo ya Yesu kwa wanafunzi wake ni kipimo cha mapendo kati ya wanafunzi. Taz Yoh 15:12,17; 2Yoh 5. 35Mkipendana, watu wote watajua kwamba nyinyi ni wanafunzi wangu.”
Yesu anatangaza kuwa Petro atamkana
(Mat 26:31-35; Marko 14:27-31; Luka 22:31-34)
36Simoni Petro akamwuliza, “Bwana, unakwenda wapi?” Yesu akajibu, “Niendako huwezi kunifuata sasa, lakini utanifuata baadaye.”#13:36 Utanifuata baadaye: Haya ni maneno yanayodokezea kifo cha Petro (21:18-19). 37Petro akamwambia “Bwana, kwa nini siwezi kukufuata sasa? Niko tayari kufa kwa ajili yako!” 38Yesu akajibu, “Je, uko tayari kweli kufa kwa ajili yangu? Kweli nakuambia, kabla jogoo hajawika utanikana mara tatu!”#13:38 Kabla jogoo hajawika utanikana mara tatu: Kwa vile jogoo huwika wakati wa mapambazuko Yesu alitaka kusema kwamba Petro atamkana mara tatu kabla ya jua kuchomoza.
Iliyochaguliwa sasa
Yohane 13: BHNTLK
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Copyright The Bible Society of Tanzania, 1993
The Bible Society of Kenya 1993