Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ufunuo 5:1-9

Ufunuo 5:1-9 SRUV

Kisha nikaona katika mkono wa kulia wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi kitabu kilichoandikwa ndani na nyuma, kimetiwa mihuri saba. Nikaona malaika mwenye nguvu akihubiri kwa sauti kuu, Ni nani anayestahili kukifungua kitabu, na kuivunja mihuri yake? Wala hapakuwa na mtu mbinguni, wala juu ya nchi, wala chini ya nchi, aliyeweza kukifungua kitabu hicho, wala kukitazama. Nami nikalia sana kwa kuwa hapakuonekana mtu astahiliye kukifungua kitabu hicho, wala kukitazama. Na mmojawapo wa wale wazee akaniambia, Usilie; tazama, Simba aliye wa kabila la Yuda, Shina la Daudi, yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na ile mihuri yake saba. Nikaona katikati ya kile kiti cha enzi na wale wenye uhai wanne, na katikati ya wale wazee, Mwana-kondoo amesimama, alikuwa kana kwamba amechinjwa, mwenye pembe saba na macho saba, ambazo ni Roho saba za Mungu zilizotumwa katika dunia yote. Akaja, akakitwaa kile kitabu katika mkono wa kulia wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi. Hata alipokitwaa kile kitabu, hao wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele za Mwana-kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambayo ni maombi ya watakatifu. Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuifungua mihuri yake; kwa kuwa ulichinjwa, ukawa fidia kwa Mungu na kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa

Soma Ufunuo 5

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Ufunuo 5:1-9