Ufunuo 19:7-8
Ufunuo 19:7-8 SRUV
Na tufurahi, tukashangilie, tukampe utukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana-kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari. Naye ameruhusiwa kuvikwa kitani nzuri, ing'aayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu.