Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 98:1-7

Zaburi 98:1-7 SRUV

Mwimbieni BWANA wimbo mpya, Kwa maana ametenda mambo ya ajabu. Mkono wa kulia, Na mkono wake mtakatifu umemtendea wokovu. BWANA ameufunua wokovu wake, Machoni pa mataifa ameidhihirisha haki yake. Amezikumbuka rehema zake, Na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli. Miisho yote ya dunia imeuona Wokovu wa Mungu wetu. Mshangilieni BWANA, nchi yote, Inueni sauti, imbeni kwa furaha, imbeni sifa. Mwimbieni BWANA sifa kwa kinubi, Kwa kinubi na sauti tamu. Kwa panda na sauti ya baragumu. Shangilieni mbele za Mfalme, BWANA. Bahari na ivume na vyote viijazavyo, Ulimwengu nao wanaokaa ndani yake.

Soma Zaburi 98