Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 98:1-7

Zab 98:1-7 SUV

Mwimbieni BWANA wimbo mpya, Kwa maana ametenda mambo ya ajabu. Mkono wa kuume wake mwenyewe, Mkono wake mtakatifu umemtendea wokovu. BWANA ameufunua wokovu wake, Machoni pa mataifa ameidhihirisha haki yake. Amezikumbuka rehema zake, Na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli. Miisho yote ya dunia imeuona Wokovu wa Mungu wetu. Mshangilieni BWANA, nchi yote, Inueni sauti, imbeni kwa furaha, imbeni zaburi. Mwimbieni BWANA zaburi kwa kinubi, Kwa kinubi na sauti ya zaburi. Kwa panda na sauti ya baragumu. Shangilieni mbele za Mfalme, BWANA. Bahari na ivume na vyote viijazavyo, Ulimwengu nao wanaokaa ndani yake.

Soma Zab 98

Verse Image for Zab 98:1-7

Zab 98:1-7 - Mwimbieni BWANA wimbo mpya,
Kwa maana ametenda mambo ya ajabu.
Mkono wa kuume wake mwenyewe,
Mkono wake mtakatifu umemtendea wokovu.
BWANA ameufunua wokovu wake,
Machoni pa mataifa ameidhihirisha haki yake.
Amezikumbuka rehema zake,
Na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli.
Miisho yote ya dunia imeuona
Wokovu wa Mungu wetu.
Mshangilieni BWANA, nchi yote,
Inueni sauti, imbeni kwa furaha, imbeni zaburi.
Mwimbieni BWANA zaburi kwa kinubi,
Kwa kinubi na sauti ya zaburi.
Kwa panda na sauti ya baragumu.
Shangilieni mbele za Mfalme, BWANA.
Bahari na ivume na vyote viijazavyo,
Ulimwengu nao wanaokaa ndani yake.