Zaburi 84:1-4
Zaburi 84:1-4 SRUV
Maskani zako zapendeza kama nini, Ee BWANA wa majeshi! Nafsi yangu imezionea shauku nyua za BWANA, Naam, na kuzikondea. Moyo wangu na mwili wangu Vinamlilia Mungu aliye hai. Hata Shomoro ameona nyumba, Na mbayuwayu amejipatia kiota, Alipoweka makinda yake, Kwenye madhabahu zako, Ee BWANA wa majeshi, Mfalme wangu na Mungu wangu. Heri wakaao nyumbani mwako, Wanakuhimidi daima.