Zaburi 84:1-4
Zaburi 84:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Jinsi gani yanavyopendeza makao yako, ee Mwenyezi-Mungu wa majeshi! Nafsi yangu yatamani mno maskani ya Mwenyezi-Mungu! Moyo na mwili wangu wote wamshangilia Mungu aliye hai. Hata shomoro wamepata makao yao, mbayuwayu wamejenga viota vyao, humo wameweka makinda yao, katika madhabahu zako, ee Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mfalme wangu na Mungu wangu! Heri wale wanaokaa nyumbani mwako, wakiimba daima sifa zako.
Zaburi 84:1-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Maskani zako zapendeza kama nini, Ee BWANA wa majeshi! Nafsi yangu imezionea shauku nyua za BWANA, Naam, na kuzikondea. Moyo wangu na mwili wangu Vinamlilia Mungu aliye hai. Hata Shomoro ameona nyumba, Na mbayuwayu amejipatia kiota, Alipoweka makinda yake, Kwenye madhabahu zako, Ee BWANA wa majeshi, Mfalme wangu na Mungu wangu. Heri wakaao nyumbani mwako, Wanakuhimidi daima.
Zaburi 84:1-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Maskani zako zapendeza kama nini, Ee BWANA wa majeshi! Nafsi yangu imezionea shauku nyua za BWANA, Naam, na kuzikondea. Moyo wangu na mwili wangu Vinamlilia Mungu aliye hai. Shomoro naye ameona nyumba, Na mbayuwayu amejipatia kioto, Alipoweka makinda yake, Kwenye madhabahu zako, Ee BWANA wa majeshi, Mfalme wangu na Mungu wangu. Heri wakaao nyumbani mwako, Wanakuhimidi daima.
Zaburi 84:1-4 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ee BWANA Mwenye Nguvu Zote, makao yako yapendeza kama nini! Nafsi yangu inatamani sana, naam, hata kuona shauku, kwa ajili ya nyua za BWANA; moyo wangu na mwili wangu vinamlilia Mungu Aliye Hai. Hata shomoro amejipatia makao, mbayuwayu amejipatia kiota mahali awezapo kuweka makinda yake: mahali karibu na madhabahu yako, Ee BWANA Mwenye Nguvu Zote, Mfalme wangu na Mungu wangu. Heri wale wanaokaa nyumbani mwako, wanaokusifu wewe daima.