Zab 84:1-4
Zab 84:1-4 SUV
Maskani zako zapendeza kama nini, Ee BWANA wa majeshi! Nafsi yangu imezionea shauku nyua za BWANA, Naam, na kuzikondea. Moyo wangu na mwili wangu Vinamlilia Mungu aliye hai. Shomoro naye ameona nyumba, Na mbayuwayu amejipatia kioto, Alipoweka makinda yake, Kwenye madhabahu zako, Ee BWANA wa majeshi, Mfalme wangu na Mungu wangu. Heri wakaao nyumbani mwako, Wanakuhimidi daima.