Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 77:3-12

Zaburi 77:3-12 SRUV

Nilipotaka kumkumbuka Mungu nilifadhaika; Nilipotaka kutafakari roho yangu ilizimia. Ulizishika kope za macho yangu zisifumbike; Nilitaabika nisiweze kunena. Nilifikiri habari za siku za kale, Miaka ya zamani zilizopita. Nanena na moyo wangu usiku, Nawaza moyoni mwangu, Roho yangu naipeleleza. Je! Bwana atatutupa milele na milele? Asiwe na fadhili kwetu kamwe? Rehema zake zimekoma hata milele? Ahadi yake imekwisha hata vizazi vyote? Mungu amesahau fadhili zake? Amezuia kwa hasira rehema zake? Nikasema, Ndio udhaifu wangu huo; Lakini nitaikumbuka miaka ya mkono wa kulia wake Aliye Juu. Nitayakumbuka matendo ya BWANA; Naam, nitayakumbuka maajabu yako ya kale. Pia nitaitafakari kazi yako yote; Nitaziwaza habari za matendo yako.

Soma Zaburi 77