Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 52

52
Hukumu kwa waongo
Kwa mwimbishaji. Utenzi wa Daudi, wakati Doegi, Mwedomu alipomwendea Sauli na kumwambia, “Daudi ameingia nyumbani mwa Ahimeleki.”
1 # 1 Sam 22:9-10; 21:7 Kwa nini kujisifia uovu, Ewe jabari?
Wema wa Mungu upo sikuzote.
2 # Zab 50:19; Mit 12:18; Zab 59:7 Ulimi wako watunga madhara,
Kama wembe mkali, Ewe mwenye hila.
3 # Yer 9:4 Umependa mabaya kuliko mema,
Na uongo kuliko kusema kweli.
4Umependa maneno yote ya kupoteza watu,
Ewe ulimi wenye hila.
5 # Mit 2:22 Lakini Mungu atakuharibu hata milele;
Atakuondolea mbali;
Atakunyakua hemani mwako;
Atakung'oa katika nchi ya walio hai.
6 # Ayu 22:19; Zab 58:10 Nao wenye haki wataona;
Wataingiwa na hofu na kumcheka;
7 # Ayu 31:24,25; Zab 49:6 Kumbe! Huyu ndiye mtu yule,
Asiyemfanya Mungu kuwa kimbilio lake.
Aliutumainia wingi wa mali zake,
Na kufanya mali kimbilio lake.
8 # Zab 92:13 Bali mimi ni kama mzeituni
Umeao katika nyumba ya Mungu.
Nazitumainia fadhili za Mungu milele na milele.
9 # Zab 54:6 Nitakushukuru milele kwa maana umetenda;
Nitalingojea jina lako kwa kuwa ni jema;
Mbele ya wacha Mungu wako.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 52: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha