Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 51:1-13

Zaburi 51:1-13 SRUV

Ee Mungu, unirehemu, kulingana na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, Uyafute makosa yangu. Unioshe kabisa uovu wangu, Unitakase dhambi zangu. Maana nimejua mimi makosa yangu Na dhambi yangu iko mbele yangu daima. Nimekutenda dhambi Wewe peke yako, Na kufanya maovu mbele za macho yako. Wewe ujulikane kuwa una haki unenapo, Na kuwa safi utoapo hukumu. Tazama, nikazaliwa nikiwa na hatia; Mama yangu akanichukua mimba nikiwa na dhambi. Tazama, wapendezwa na kweli iliyo moyoni; Nawe utanifundisha hekima kwa siri, Unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi, Unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji. Unifanye kusikia furaha na shangwe, Mifupa uliyoiponda ifurahi. Usitiri uso wako usitazame dhambi zangu; Uzifute hatia zangu zote. Ee Mungu, uniumbie moyo safi, Uifanye upya na kuithibiti roho yangu. Usinitenge na uso wako, Wala roho yako mtakatifu usiniondolee. Unirudishie furaha ya wokovu wako; Unitegemeze kwa roho ya upendo. Nitawafundisha wakosaji njia zako, Na wenye dhambi watarejea kwako.

Soma Zaburi 51

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zaburi 51:1-13

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha