Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 47

47
Utawala wa Mungu juu ya mataifa
Kwa mwimbishaji. Ya Wakorahi. Zaburi.
1Enyi watu wote, pigeni makofi,
Mpigieni Mungu kelele kwa Sauti ya shangwe.
2 # Kum 7:21; Neh 1:5; Mal 1:14 Kwa kuwa BWANA Aliye Juu, mwenye kuogofya,
Ndiye mfalme mkuu juu ya dunia yote.
3 # Zab 18:47 Amewatiisha watu wa nchi chini yetu,
Na mataifa chini ya miguu yetu.
4 # 1 Pet 1:4 Ametuchagulia urithi wetu,
Fahari ya Yakobo ampendaye.
5 # Zab 24:7-10; Mdo 1:9; Efe 4:8-10; 1 Tim 3:16 Mungu amepaa kwa kelele za shangwe,
BWANA kwa sauti ya baragumu.
6Mwimbieni Mungu sifa, imbeni sifa;
Imbeni sifa kwa mfalme wetu, imbeni sifa.
7 # Zek 14:9; 1 Kor 14:15 Maana Mungu ndiye mfalme wa dunia yote,
Imbeni kwa zaburi.
8Mungu ayatawala mataifa,
Mungu ameketi katika kiti chake kitakatifu.
9Wakuu wa watu wamekusanyika,
Kama watu wa Mungu wa Abrahamu.
Maana ngao za dunia zina Mungu,
Ametukuka sana.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 47: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha