Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 46

46
Ulinzi wa Mungu kwa mji na watu wake
Kwa mwimbishaji. Ya Wakorahi. Kwa mtindo wa Alamothi. Wimbo.
1Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu,
Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.
2Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi,
Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari.
3Maji yake yajapovuma na kuumuka,
Ijapopepesuka milima kwa kiburi chake.
4 # Isa 8:7; Ufu 22:1; 2 Nya 6:6; Zab 48:1; Isa 60:14; Ebr 12:22 Kuna mto, vijito vyake vyaufurahisha mji wa Mungu,
Patakatifu pa maskani zake Aliye Juu.
5 # Kum 23:14; Isa 12:6; Eze 43:7 Mungu yu katikati ya mji hautatetemeshwa;
Mungu atausaidia asubuhi na mapema.
6Mataifa yanaghadhibika na falme kutetemeka;
Anatoa sauti yake, nchi inayeyuka.
7BWANA wa majeshi yu pamoja nasi,
Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.
8Njoni muyatazame matendo ya BWANA,
Jinsi alivyofanya ukiwa katika nchi.
9Avikomesha vita hata mwisho wa dunia;
Avunja uta, akata mkuki, achoma moto magari.
10 # Kut 14:13; Isa 2:11 Tulieni, mjue ya kuwa Mimi ni Mungu,
Nitakuzwa katika mataifa, nitakuzwa katika nchi.
11BWANA wa majeshi yu pamoja nasi,
Mungu wa Yakobo ni kimbilio#46:11 Au ngome yetu. letu.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 46: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha