Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 40

40
Shukrani kwa kuponywa na sala ya kutaka msaada
Kwa mwimbishaji. Ya Daudi. Zaburi.
1Nilimngoja BWANA kwa subira,
Akaniinamia na kusikia kilio changu.
2Akanipandisha toka shimo la uharibifu,
Toka udongo wa utelezi;
Akaisimamisha miguu yangu mwambani,
Akaziimarisha hatua zangu.
3Akatia wimbo mpya kinywani mwangu,
Ndio sifa zake Mungu wetu.
Wengi wataona na kuogopa,
Nao watamtumainia BWANA.
4 # Zab 2:12 Heri aliyemfanya BWANA kuwa tumaini lake,
Wala hakuwaelekea wenye kiburi,
Wala hao wanaogeukia uongo.
5 # Isa 55:8 Ee BWANA, Mungu wangu, umefanya kwa wingi
Miujiza yako na mawazo yako kwetu;
Hakuna awezaye kufananishwa nawe;
Kama ningependa kuyatangaza na kuyahubiri,
Ni mengi sana hayahesabiki.
6 # Ebr 10:5-7; Hos 6:6; Mt 9:13 Dhabihu na matoleo hukupendezwa nazo,
Umetuzidishia ila masikio,
Kafara na sadaka za dhambi hukuzitaka.
7 # Lk 24:44; Yn 5:39; Mdo 10:43; Ebr 10:7 Ndipo niliposema, Tazama nimekuja,
(Katika gombo la kitabu nimeandikiwa,)
8 # Ayu 23:12; Yer 15:16; Yn 4:34; Rum 7:22 Kuyafanya mapenzi yako,
Ee Mungu wangu, ndiyo furaha yangu;
Naam, sheria yako imo moyoni mwangu.
9 # Zab 139:2 Nimehubiri habari za haki katika kusanyiko kubwa.
Sikuizuia midomo yangu; Ee BWANA, unajua.
10 # Mdo 20:20; Rum 1:16,17; Flp 3:9 Sikusitiri haki yako moyoni mwangu;
Nimetangaza uaminifu wako na wokovu wako.
Sikuficha fadhili zako wala kweli yako
Katika kusanyiko kubwa.
11 # Zab 43:3 Nawe, BWANA, usinizuilie rehema zako,
Fadhili zako na kweli yako na zinihifadhi daima.
12 # Zab 38:4 Kwa maana mabaya yasiyohesabika
Yamenizunguka mimi.
Maovu yangu yamenipata,
Wala siwezi kuona.
Yamezidi kuliko nywele za kichwa changu,
Nami nimevunjika moyo.
13Ee BWANA, uwe radhi kuniokoa,
Ee BWANA, unisaidie hima.
14Waaibike na wafedheheke,
Wote wanaotaka kuniua.
Warudishwe nyuma, watahayarishwe,
Wapendezwao na shari yangu.
15Wafadhaike kwa aibu yao,
Wanaoniambia Ewe! Ewe!
16Washangilie na wakufurahie,
Wote wakutafutao.
Waupendao wokovu wako
Waseme daima, BWANA ni Mkuu.
17 # Neh 5:19; Yon 1:6 Nami ni maskini na mhitaji,
Bwana atanitunza.
Ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu,
Ee Mungu wangu, usikawie.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 40: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha