Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 38:11-22

Zaburi 38:11-22 SRUV

Wanipendao na rafiki zangu wanasimama mbali na pigo langu; Na jamaa zangu wanasimama mbali. Nao wanaoutafuta uhai wangu hutega mitego; Nao wanaotaka kunidhuru hunena mabaya; Na kufikiri hila mchana kutwa. Lakini kama kiziwi sisikii, Nami ni kama bubu asiyefumbua kinywa chake. Naam, nimekuwa kama mtu asiyesikia, Ambaye hamna ubishi kinywani mwake. Kwa kuwa nakungoja Wewe, BWANA, Wewe utajibu, Ee Bwana, Mungu wangu. Maana nilisema, Wasije wakanifurahia; Wale wanaojitukuza juu yangu Mguu wangu unapoteleza. Kwa maana mimi ni karibu na kusita, Na maumivu yangu yako mbele yangu daima. Kwa maana nitaungama uovu wangu, Na kusikitika kwa dhambi zangu. Lakini walio adui zangu bila sababu wana nguvu, Nao wanaonichukia bure wamekuwa wengi. Naam, wakilipa mabaya kwa mema, Huwa adui zangu kwa kuwa nilifuata lililo jema. Wewe, BWANA, usiniache, Mungu wangu, usijitenge nami. Ufanye haraka kunisaidia, Ee Bwana, wokovu wangu.

Soma Zaburi 38