Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 26:1-12

Zaburi 26:1-12 SRUV

Ee BWANA, unihukumu mimi, Maana nimekwenda kwa ukamilifu wangu, Nami nimemtumaini BWANA bila wasiwasi. Ee BWANA, unijaribu na kunipima; Unisafishe akili yangu na moyo wangu. Maana fadhili zako zi mbele ya macho yangu, Nami nimekwenda katika kweli yako. Sikai pamoja na watu waovu, Wala sitaingia kuwa pamoja na wanafiki. Nimelichukia kusanyiko la watenda mabaya, Wala sitaketi pamoja na watu waovu. Nitanawa mikono yangu bila ya kuwa na hatia, Na kuizunguka madhabahu yako, Ee BWANA Ili niitangaze sauti ya kushukuru, Na kuzisimulia kazi zako za ajabu. BWANA, nimependa makao ya nyumba yako, Na mahali pa maskani ya utukufu wako. Usiiondoe nafsi yangu pamoja na wakosaji, Wala uhai wangu pamoja na wauaji. Mikononi mwao mna madhara, Na mkono wao wa kulia umejaa rushwa. Ila mimi nitakwenda kwa ukamilifu wangu; Unikomboe, unifanyie fadhili. Mguu wangu umesimama palipo sawa; Katika kusanyiko kuu nitamhimidi BWANA.

Soma Zaburi 26