Zaburi 26:1-12
Zaburi 26:1-12 Biblia Habari Njema (BHN)
Ee Mwenyezi-Mungu, unitetee, maana nimeishi bila hatia, nimekutumainia wewe bila kusita. Unijaribu, ee Mwenyezi-Mungu, na kunipima; uchunguze moyo wangu na akili zangu. Fadhili zako ziko mbele ya macho yangu, ninaishi kutokana na uaminifu wako. Sijumuiki na watu wapotovu; sishirikiani na watu wanafiki. Nachukia mikutano ya wabaya; wala sitajumuika na waovu. Nanawa mikono yangu kuonesha sina hatia, na kuizunguka madhabahu yako, ee Mwenyezi-Mungu, nikiimba wimbo wa shukrani, na kusimulia matendo yako yote ya ajabu. Ee Mwenyezi-Mungu, napenda makao yako, mahali unapokaa utukufu wako. Usiniangamize pamoja na wenye dhambi, wala usinitupe pamoja na wauaji, watu ambao matendo yao ni maovu daima, watu ambao wamejaa rushwa. Lakini mimi ninaishi kwa unyofu; unihurumie na kunikomboa. Mimi nimesimama mahali palipo imara; nitamsifu Mwenyezi-Mungu katika kusanyiko kubwa.

Zaburi 26:1-12 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee BWANA, unihukumu mimi, Maana nimekwenda kwa ukamilifu wangu, Nami nimemtumaini BWANA bila wasiwasi. Ee BWANA, unijaribu na kunipima; Unisafishe akili yangu na moyo wangu. Maana fadhili zako zi mbele ya macho yangu, Nami nimekwenda katika kweli yako. Sikai pamoja na watu waovu, Wala sitaingia kuwa pamoja na wanafiki. Nimelichukia kusanyiko la watenda mabaya, Wala sitaketi pamoja na watu waovu. Nitanawa mikono yangu bila ya kuwa na hatia, Na kuizunguka madhabahu yako, Ee BWANA Ili niitangaze sauti ya kushukuru, Na kuzisimulia kazi zako za ajabu. BWANA, nimependa makao ya nyumba yako, Na mahali pa maskani ya utukufu wako. Usiiondoe nafsi yangu pamoja na wakosaji, Wala uhai wangu pamoja na wauaji. Mikononi mwao mna madhara, Na mkono wao wa kulia umejaa rushwa. Ila mimi nitakwenda kwa ukamilifu wangu; Unikomboe, unifanyie fadhili. Mguu wangu umesimama palipo sawa; Katika kusanyiko kuu nitamhimidi BWANA.
Zaburi 26:1-12 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ee BWANA, unihukumu mimi, Maana nimekwenda kwa ukamilifu wangu, Nami nimemtumaini BWANA bila wasiwasi. Ee BWANA, unijaribu na kunipima; Unisafishe mtima wangu na moyo wangu. Maana fadhili zako zi mbele ya macho yangu, Nami nimekwenda katika kweli yako. Sikuketi pamoja na watu wa ubatili, Wala sitaingia mnamo wanafiki. Nimelichukia kusanyiko la watenda mabaya, Wala sitaketi pamoja na watu waovu. Nitanawa mikono yangu kwa kutokuwa na hatia, Na kuizunguka madhabahu yako, Ee BWANA Ili niitangaze sauti ya kushukuru, Na kuzisimulia kazi zako za ajabu. BWANA, nimependa makao ya nyumba yako, Na mahali pa maskani ya utukufu wako. Usiiondoe nafsi yangu pamoja na wakosaji, Wala uhai wangu pamoja na watu wa damu. Mikononi mwao mna madhara, Na mkono wao wa kuume umejaa rushwa. Ila mimi nitakwenda kwa ukamilifu wangu; Unikomboe, unifanyie fadhili. Mguu wangu umesimama palipo sawa; Katika makusanyiko nitamhimidi BWANA.
Zaburi 26:1-12 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Ee Mwenyezi Mungu, nithibitishe katika haki, maana nimeishi maisha yasiyo na lawama; nimemtumainia Mwenyezi Mungu bila kusitasita. Ee Mwenyezi Mungu, unijaribu, unipime, uuchunguze moyo wangu na mawazo yangu; kwa maana upendo wako uko mbele yangu daima, nami natembea siku zote katika kweli yako. Siketi pamoja na watu wadanganyifu, wala siandamani na wanafiki, ninachukia kusanyiko la watenda maovu, na ninakataa kuketi pamoja na waovu. Ninanawa mikono yangu kwa kuwa sina hatia, naikaribia madhabahu yako, Ee Mwenyezi Mungu, nikitangaza sifa yako kwa sauti kubwa, huku nikisimulia matendo yako ya ajabu. Ee Mwenyezi Mungu, naipenda nyumba yako unakoishi, mahali pale utukufu wako hukaa. Usiiondoe nafsi yangu pamoja na watenda dhambi, wala uhai wangu pamoja na wanaomwaga damu, ambao mikononi mwao kuna mipango miovu, ambao mikono yao ya kuume imejaa rushwa. Bali mimi ninaishi maisha yasiyo na lawama; nikomboe na unihurumie. Miguu yangu imesimama katika uwanja tambarare; katika kusanyiko kuu nitamsifu Mwenyezi Mungu.