Zaburi 25:1-10
Zaburi 25:1-10 SRUV
Ee BWANA, nakuinulia nafsi yangu, Ee Mungu wangu, Nimekutumainia Wewe, nisiaibike, Adui zangu wasifurahi kwa kunishinda. Naam, wakungojao hawataaibika hata mmoja; Wataaibika watendao uhaini bila sababu. Ee BWANA, unijulishe njia zako, Unifundishe mapito yako, Uniongoze katika kweli yako, Na kunifundisha. Maana Wewe ndiwe Mungu wa wokovu wangu, Nakungoja Wewe mchana kutwa. Ee BWANA, kumbuka rehema zako na fadhili zako, Maana zimekuwako tokea zamani. Usiyakumbuke makosa ya ujana wangu, Wala maasi yangu. Unikumbuke kwa kadiri ya fadhili zako, Ee BWANA kwa ajili ya wema wako. BWANA yu mwema, mwenye adili, Kwa hiyo atawafundisha wenye dhambi njia. Wenye upole atawaongoza katika haki, Wenye upole atawafundisha njia yake. Njia zote za BWANA ni fadhili na kweli, Kwao walishikao agano lake na shuhuda zake.