Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 25:1-10

Zaburi 25:1-10 NEN

Kwako wewe, Ee BWANA, nainua nafsi yangu, ni wewe ninayekutumainia, Ee Mungu wangu. Usiniache niaibike, wala usiache adui zangu wakanishinda. Kamwe hakuna hata mmoja anayekutegemea atakayeaibishwa, bali wataaibishwa wafanyao hila bila sababu. Nionyeshe njia zako, Ee BWANA, nifundishe mapito yako, niongoze katika kweli yako na kunifundisha, kwa maana wewe ni Mungu Mwokozi wangu, nalo tumaini langu liko kwako wakati wote. Kumbuka, Ee BWANA, rehema zako kuu na upendo, kwa maana zimekuwepo tangu zamani. Usizikumbuke dhambi za ujana wangu wala njia zangu za uasi, sawasawa na upendo wako unikumbuke, kwa maana wewe ni mwema, Ee BWANA. BWANA ni mwema na mwenye adili, kwa hiyo huwafundisha wenye dhambi njia zake. Huwaongoza wanyenyekevu katika haki, naye huwafundisha njia yake. Njia zote za BWANA ni za upendo na uaminifu kwa wale wanaoshika shuhuda za agano lake.