Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 147:2-11

Zaburi 147:2-11 SRUV

BWANA ndiye aijengaye Yerusalemu, Huwakusanya waliotawanyika wa Israeli. Huwaponya waliopondeka moyo, Na kuyaganga majeraha yao. Huihesabu idadi ya nyota, Huzipa zote majina. Bwana wetu ni mkuu na mwingi wa nguvu, Akili zake hazina mpaka. BWANA huwategemeza wenye upole, Huwaangusha chini wenye jeuri. Mwimbieni BWANA kwa kushukuru, Mwimbieni Mungu wetu kwa kinubi. Huzifunika mbingu kwa mawingu, Huitengenezea nchi mvua, Na kuichipusha nyasi milimani. Humpa mnyama chakula chake, Wana-kunguru waliao. Hapendezwi na nguvu za farasi, Wala hairidhii miguu ya mkimbiaji. BWANA huwaridhia wao wamchao, Na kuzitarajia fadhili zake.

Soma Zaburi 147

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zaburi 147:2-11