Zaburi 119:158-160
Zaburi 119:158-160 SRUV
Nimewaona watendao uhaini nikachukizwa, Kwa sababu hawakulitii neno lako. Uangalie niyapendavyo mausia yako, Ee BWANA, unihuishe sawasawa na fadhili zako. Jumla ya neno lako ni kweli, Na kila hukumu ya haki yako ni ya milele.