Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mithali 27:23-27

Mithali 27:23-27 SRUV

Fanya bidii kuijua hali ya makundi yako; Na kuwaangalia sana ng'ombe wako. Kwa maana mali haziwi za milele; Na taji je! Ladumu tangu kizazi hata kizazi? Manyasi hukatwa, na majani mabichi huchipua, Na mboga ya mlimani hukusanywa. Wana-kondoo hufaa kwa mavazi yako; Na mbuzi ni thamani ya shamba. Tena yatakuwapo maziwa ya mbuzi, Ya kukutosha kwa chakula chako, Na chakula cha watu wa nyumbani mwako, Na posho la vijakazi vyako.

Soma Mithali 27

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Mithali 27:23-27