Methali 27:23-27
Methali 27:23-27 Biblia Habari Njema (BHN)
Angalia vizuri hali ya mifugo yako; tunza vizuri wanyama wako. Maana utajiri haudumu milele, wala taji haidumu vizazi vyote. Baada ya kukata nyasi na kuzihifadhi, kata majani toka milimani, huku nyasi zinachipua upya. Kondoo watakupatia sufu kwa mavazi, mbuzi nao utauza na kujinunulia mashamba; watakupa maziwa ya kukutosha wewe na jamaa yako, na kwa ajili ya watumishi wako wa kike.
Methali 27:23-27 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Fanya bidii kuijua hali ya makundi yako; Na kuwaangalia sana ng'ombe wako. Kwa maana mali haziwi za milele; Na taji je! Ladumu tangu kizazi hata kizazi? Manyasi hukatwa, na majani mabichi huchipua, Na mboga ya mlimani hukusanywa. Wana-kondoo hufaa kwa mavazi yako; Na mbuzi ni thamani ya shamba. Tena yatakuwapo maziwa ya mbuzi, Ya kukutosha kwa chakula chako, Na chakula cha watu wa nyumbani mwako, Na posho la vijakazi vyako.
Methali 27:23-27 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Fanya bidii kuijua hali ya makundi yako; Na kuwaangalia sana ng’ombe zako. Kwa maana mali haziwi za milele; Na taji je! Yadumu tangu kizazi hata kizazi? Manyasi huchukuliwa, na majani mabichi huonekana, Na maboga ya milimani hukusanyika. Wana-kondoo hufaa kwa mavazi yako; Na mbuzi ni thamani ya shamba Tena yatakuwapo maziwa ya mbuzi, Ya kukutosha kwa chakula chako, Na chakula cha watu wa nyumbani mwako, Na posho la vijakazi vyako.
Methali 27:23-27 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Hakikisha kuwa unajua hali ya makundi yako ya kondoo na mbuzi, angalia kwa bidii ngʼombe zako. Kwa kuwa utajiri haudumu milele, nayo taji haidumu vizazi vyote. Wakati majani makavu yameondolewa na mapya yamechipua, nayo majani toka milimani yamekusanywa, wana-kondoo watakupatia mavazi na mbuzi thamani ya shamba. Utakuwa na maziwa mengi ya mbuzi kukulisha wewe na jamaa yako, na kuwalisha watumishi wako wa kike.