Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mithali 11:1-11

Mithali 11:1-11 SRUV

Mizani ya udanganyifu ni chukizo kwa BWANA; Bali vipimo vilivyo sawasawa humpendeza. Kijapo kiburi ndipo ijapo aibu; Bali hekima hukaa na wanyenyekevu. Ukamilifu wao wenye haki utawaongoza Bali ukaidi wao wenye fitina utawaangamiza. Mali hazifaidii kitu siku ya ghadhabu; Bali haki huokoa na mauti. Haki yake mtu mkamilifu itamwongoza njia yake; Bali mtu mwovu ataanguka kwa uovu wake. Haki yao wenye haki itawaokoa; Bali wafanyao fitina watanaswa kwa hila yao wenyewe. Mtu mwovu atakapokufa, taraja lake linapotea; Na matumaini ya uovu huangamia. Mwenye haki huokolewa katika dhiki, Na mtu mwovu ataiingia badala yake. Asiyemcha Mungu humpoteza jirani yake kwa kinywa chake; Bali wenye haki watapona kwa maarifa. Wenye haki wasitawipo, mji hufurahi; Waovu wanapoangamia, watu hushangilia. Mji hutukuzwa kwa mbaraka wa mwenye haki; Bali mji hupinduliwa kwa kinywa cha mwovu.

Soma Mithali 11