Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Obadia UTANGULIZI

UTANGULIZI
Maana ya jina Obadia katika lugha ya Kiebrania ni “mtumishi wa BWANA” au “mwabudu BWANA”. Kitabu hiki hakitaji kiliandikwa lini, aidha mwandishi alipoishi sio yakini na mambo kadhaa ya ujumbe wake yanasimuliwa katika vitabu vingine vya manabii.
Ujumbe wa Obadia unahusu taifa la Edomu. Edomu maana yake ni “nyekundu” nalo ni jina aliloitwa Esau, wazao wake na nchi walimoishi (Mwa 36:1,8-9; 25:15,30). Kwa kuwa Israeli ilitawala Edomu baadaye Waedomi wakajikomba kulikuweko kutoelewana hata uhasama. Yuda ilipotekwa, Yerusalemu ukabomolewa, wakazi wake wakachukuliwa mateka, Edomu walifurahi wakajiunga na adui wa Yuda kupora mali ya Yuda. Ujumbe wa nabii Obadia unaeleza hali ya uhasama na mafarakano yaliyokuwapo kati ya mataifa ndugu. Pia ukatoa hukumu ya Mungu kwa Edomu. “Siku ya BWANA” ni wakati ambapo taifa la Mungu litalipiza kisasi kwa Edomu.
Yaliyomo:
1. Mungu atashusha kiburi cha Edomu, Aya 1-4
2. Mungu ataangamiza nchi ya Edomu, Aya 5-9
3. Sababu za kuangamizwa Edomu, Aya 10-16
4. Israeli na Yuda wataimarishwa, Aya 17-21

Iliyochaguliwa sasa

Obadia UTANGULIZI: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha