Ayubu 33:1-7
Ayubu 33:1-7 SRUV
Lakini, Ayubu, nakuomba usikilize hoja yangu, Ukayasikilize maneno yangu yote. Tazama basi, nimefunua kinywa changu, Ulimi wangu umenena kinywani mwangu. Maneno yangu yatatamka uelekevu wa moyo wangu; Na hayo niyajuayo midomo yangu itayanena kwa unyofu. Roho ya Mungu imeniumba, Na pumzi za Mwenyezi hunipa uhai. Ikiwa unaweza, nijibu; Yapange maneno yako sawasawa mbele yangu, usimame. Tazama, mimi ni mbele ya Mungu kama ulivyo wewe; Mimi nami nilifinyangwa katika udongo. Tazama, utisho wangu hautakutia hofu wewe, Wala sitakulemea kwa uzito.