Yobu 33:1-7
Yobu 33:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)
“Sasa, Yobu, sikiliza hoja yangu; sikiliza maneno yangu yote. Tazama, nafumbua kinywa changu, naam, ulimi wangu utasema. Nitasema kadiri ya unyofu wa moyo wangu; ninayoyajua nitayasema kwa uaminifu. Roho ya Mungu iliniumba, nayo pumzi ya Mungu Mwenye Nguvu yanipa uhai. Nijibu, kama unaweza. Panga hoja zako vizuri mbele yangu, ushike msimamo wako. Wewe na mimi ni sawa mbele ya Mungu; mimi pia niliumbwa kwa sehemu ya udongo. Kwa hiyo huna sababu ya kuniogopa; maneno yangu mazito hayatakulemea.
Yobu 33:1-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Lakini, Ayubu, nakuomba usikilize hoja yangu, Ukayasikilize maneno yangu yote. Tazama basi, nimefunua kinywa changu, Ulimi wangu umenena kinywani mwangu. Maneno yangu yatatamka uelekevu wa moyo wangu; Na hayo niyajuayo midomo yangu itayanena kwa unyofu. Roho ya Mungu imeniumba, Na pumzi za Mwenyezi hunipa uhai. Ikiwa unaweza, nijibu; Yapange maneno yako sawasawa mbele yangu, usimame. Tazama, mimi ni mbele ya Mungu kama ulivyo wewe; Mimi nami nilifinyangwa katika udongo. Tazama, utisho wangu hautakutia hofu wewe, Wala sitakulemea kwa uzito.
Yobu 33:1-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Walakini, Ayubu, nakuomba usikilize matamko yangu, Ukayasikilize maneno yangu yote. Tazama basi, nimefunua kinywa changu, Ulimi wangu umenena kinywani mwangu. Maneno yangu yatatamka uelekevu wa moyo wangu; Na hayo niyajuayo midomo yangu itayanena kwa unyofu. Roho ya Mungu imeniumba, Na pumzi za Mwenyezi hunipa uhai. Kwamba waweza, nijibu; Yapange maneno yako sawasawa mbele yangu, usimame. Tazama, mimi ni mbele ya Mungu kama ulivyo wewe; Mimi nami nilifinyangwa katika udongo. Tazama, utisho wangu hautakutia hofu wewe, Wala sitakulemea kwa uzito.
Yobu 33:1-7 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Lakini Ayubu, sasa, sikiliza maneno yangu; zingatia kila kitu nitakachosema. Karibu nitafungua kinywa changu; maneno yangu yapo katika ncha ya ulimi wangu. Maneno yangu yanatoka katika moyo mnyofu; midomo yangu hunena kwa uaminifu yale niyajuayo. Roho wa Mungu ameniumba; pumzi ya Mwenyezi hunipa uhai. Unijibu basi, kama unaweza; jiandae kunikabili mimi. Mimi ni kama wewe mbele za Mungu; mimi pia nimetolewa kwenye udongo. Huna sababu ya kuniogopa, wala mkono wangu haupaswi kukulemea.