Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yohana 7:1-6, 8-10

Yohana 7:1-6 SRUV

Na baada ya hayo Yesu alikuwa akitembea katika Galilaya; maana hakutaka kutembea katika Yudea, kwa sababu Wayahudi walikuwa wakitaka kumwua. Na sikukuu ya Wayahudi, sikukuu ya vibanda, ilikuwa karibu. Basi ndugu zake wakamwambia, Ondoka hapa, uende Yudea, wanafunzi wako nao wapate kuzitazama kazi zako unazozifanya. Kwa maana hakuna mtu afanyaye mambo kwa siri, naye yeye mwenyewe anataka kujulikana. Ukifanya mambo haya, basi jidhihirishe kwa ulimwengu. Maana hata nduguze hawakumwamini. Basi Yesu akawaambia, Wakati wangu haujafika bado; ila wakati wenu sikuzote upo.

Soma Yohana 7

Yohana 7:8-10 SRUV

Pandeni ninyi kwenda kula sikukuu; mimi sipandi bado kwenda kula sikukuu hii, kwa kuwa wakati wangu haujatimia. Naye alipokwisha kuwaambia hayo, alibaki huko Galilaya. Hata ndugu zake walipokwisha kupanda kuiendea sikukuu, ndipo yeye naye alipopanda, si kwa wazi bali kana kwamba kwa siri.

Soma Yohana 7

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Yohana 7:1-6, 8-10