Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yohana 7:1-6, 8-10

Yohana 7:1-6 NEN

Baada ya mambo haya, Yesu alikwenda sehemu mbalimbali za Galilaya. Hakutaka kwenda Uyahudi kwa sababu Wayahudi huko walitaka kumuua. Sikukuu ya Vibanda ya Wayahudi ilikuwa imekaribia. Hivyo ndugu zake Yesu wakamwambia, “Ondoka hapa uende Uyahudi ili wanafunzi Wako wapate kuona miujiza unayofanya. Mtu anayetaka kujulikana hafanyi mambo yake kwa siri. Kama unafanya mambo haya, jionyeshe kwa ulimwengu.” Hata ndugu zake mwenyewe hawakumwamini. Yesu akawaambia, “Wakati wangu bado haujawadia, lakini wakati wenu upo siku zote.

Yohana 7:8-10 NEN

Ninyi nendeni kwenye Sikukuu, lakini mimi sitahudhuria Sikukuu hii kwa sababu wakati wangu haujawadia.” Akiisha kusema hayo, akabaki Galilaya. Lakini ndugu zake walipokwisha kuondoka kwenda kwenye Sikukuu, yeye pia alikwenda lakini kwa siri.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Yohana 7:1-6, 8-10