Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isaya 51:12-16

Isaya 51:12-16 SRUV

Mimi, naam, mimi, ndimi niwafarijiye; wewe u nani hata ukamwogopa mtu atakayekufa, na mwanadamu atakayefanywa kuwa kama majani? Ukamsahau BWANA, Muumba wako, yeye aliyezitanda mbingu, na kuiweka misingi ya dunia; nawe unaogopa daima mchana kutwa kwa sababu ya ghadhabu yake yeye aoneaye, hapo ajitayarishapo kuharibu; nayo i wapi ghadhabu yake aoneaye? Yeye aliyehamishwa na kufungwa atafunguliwa kwa haraka; wala hatakufa na kushuka shimoni, wala chakula chake hakitapunguka. Maana mimi ni BWANA, Mungu wako, niichafuaye bahari, mawimbi yake yakavuma. BWANA wa majeshi ndilo jina lake. Nami nimetia maneno yangu kinywani mwako, nami nimekusitiri katika kivuli cha mkono wangu, ili nizipande mbingu, na kuiweka misingi ya dunia, na kuuambia Sayuni, Ninyi ni watu wangu.

Soma Isaya 51

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Isaya 51:12-16