Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isaya 51:12-16

Isaya 51:12-16 NEN

“Mimi, naam mimi, ndimi niwafarijie ninyi. Ninyi ni nani hata kuwaogopa wanadamu wanaokufa, wanadamu ambao ni majani tu, kwamba mnamsahau BWANA Muumba wenu, aliyezitanda mbingu na kuiweka misingi ya dunia, kwamba mnaishi katika hofu siku zote kwa sababu ya ghadhabu ya mdhalimu, ambaye nia yake ni kuangamiza? Iko wapi basi ghadhabu ya mdhalimu? Wafungwa waliojikunyata kwa hofu watawekwa huru karibuni; hawatafia kwenye gereza lao, wala hawatakosa chakula. Kwa maana Mimi ndimi BWANA, Mungu wako, ambaye huisukasuka bahari ili mawimbi yake yangurume: BWANA Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake. Nimeweka maneno yangu kinywani mwako na kukufunika kwa uvuli wa mkono wangu: Mimi niliyeweka mbingu mahali pake, niliyeweka misingi ya dunia, niwaambiaye Sayuni, ‘Ninyi ni watu wangu.’ ”

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Isaya 51:12-16