Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Waraka kwa Waebrania 10:18-22

Waraka kwa Waebrania 10:18-22 SRUV

Basi, ondoleo la hayo likiwapo, hapana toleo tena kwa ajili ya dhambi. Basi, ndugu, kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu, njia ile aliyotuanzia iliyo mpya, iliyo hai, ipitayo katika pazia, yaani, mwili wake; na kuwa na kuhani mkuu juu ya nyumba ya Mungu; na tukaribie wenye moyo wa kweli, kwa utimilifu wa imani, hali tumenyunyiziwa mioyo tuache dhamiri mbaya, tumeoshwa miili kwa maji safi.